Yanga waingiza timu uwanjani

Saturday May 08 2021
timu ndani pic
By Ramadhan Elias

SAA 10:58 jioni kikosi cha Yanga kimeingia uwanjani na jezi za mchezo kwa maaa ya flana za njano na bukta nyeusi kwa lengo la kuanza mchezo.

Wachezaji 11 ambao ni Metacha Mnata, Adeyum Saleh, Shomari Kibwana, Bakari Mwamnyeto, Abdallah Shaibu, Mukoko Tonombe, Feisal Salum, Tuisila Kisinda, Said Ntibazonkiza, Yacouba Sogne na Michael Sarpong waliingia katika eneo la kuchezea huku wengine wakikaa benchi.

Baada ya kuingia walikaa upande mmoja wa uwanja kimafungu mafungu wakipiga stori huku wakiwasubiri wapinzani wao Simba na waamuzi wafike uwanjani hapo.

Ikumbukwe kuwa dakika chache baada ya tukio hilo tayari wachezaji wa Yanga walikuwa wameingia uwanjani hapo wakiwa na jezi za kupashia na kuondoka baada ya muda mfupi.

Si waamuzi wala wenyeji Simba walioonekana uwanjani hapo kwa wakati huo.

Advertisement