Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga SC yashtukia dili kwa Mkude, Mwanjali

Muktasari:

  • Kocha wa Simba, Joseph Omog amekuwa akifanya mabadiliko kadhaa katika kikosi chake kwa kila mechi lakini amegonga mwamba kwa nyota wanne akiwemo beki wao Mzimbabwe, Method Mwanjali

WIKIENDI iliyopita presha yote ya mashabiki wa soka, ilikuwa England kwenye mechi ya Man United na Man City. Lakini hapa Bongo ghafla upepo umehamia Oktoba Mosi ambapo Simba na Yanga zitakipiga Taifa.

Yanga ambayo ilishinda mechi zote mbili za msimu uliopita, itakuwa mwenyeji wa mchezo huo ambao piga ua kwa ubora wa Simba ya sasa na tathmini ya mechi nne zilizopita lazima kuna mastaa wanne ambao wataanza na watafanya mambo.

Kocha wa Simba, Joseph Omog amekuwa akifanya mabadiliko kadhaa katika kikosi chake kwa kila mechi lakini amegonga mwamba kwa nyota wanne akiwemo beki wao Mzimbabwe, Method Mwanjali, kipa Vincent Angban, beki Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na kiungo Jonas Mkude.

Omog tayari ametumia wachezaji 18 tofauti katika mechi nne za msimu huu huku eneo ambalo limeonekana kufanyiwa mabadiliko makubwa likiwa ni beki ya kulia ambayo nyota watatu tofauti Hamad Juma ambaye ni majeruhi, Malika Ndeule na Javier Bokungu wakiwa wamecheza.

Wachezaji ambao bado hawajacheza kabisa katika kikosi cha Omog ni pamoja na usajili mpya Emmanuel Semwanza, Ame Ally pamoja na Mussa Ndusha ambaye inadaiwa kuwa usajili wake haujakamilika. Wengine ni Abdi Banda, Awadhi Juma pamoja na kipa Manyika Peter.

Kiungo Mohammed Ibrahim ndiye aliyecheza dakika chache zaidi akiwa ametumia dakika sita tu uwanjani dhidi ya Ndanda FC ambapo aliingia katika dakika ya 84 kuchukua nafasi ya Shiza Kichuya.

Kocha msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja alisema Simba ya msimu huu ina kikosi kipana na ndiyo sababu wamekuwa wakitumia wachezaji wengi huku wote wakicheza kwa kiwango cha juu.

“Raha ya kikosi ni kuona kile kinachoanza na kinachoingia kipindi cha pili kinafanya kazi moja na ndiyo Simba ya msimu huu mchezaji anayeanza na anayeingia kipindi cha pili huwa uwezo wao unakuwa mkubwa na hiyo inasaidia kulinda viwango vyao wakitambua fika kwamba akichemka mechi moja inakuwa imekula kwake,” alisema.

Alijigamba kwamba ligi ni ngumu lakini kwa jinsi ambavyo kikosi chao kimekamilika wapo tayari kukabiliana na kila upinzani kuhakikisha wanatimiza ndoto zinazosubiriwa na mamia ya mashabiki wao wa ndani na nje ya nchini.

MZUNGU AIKUBALI SIMBA

Kocha wa African Lyon, Bernado Tavares alicheza na Yanga ikamfunga mabao 3-0 lakini ameikaushia timu hiyo na kudai kuwa Simba ndiyo habari ya mjini na inatandaza soka la kufa mtu.

“Niwe tu muwazi, napenda namna Simba wanavyocheza, wanacheza vizuri, wanatengeneza nafasi na wanafunga mabao, soka lao linavutia,” alisema Tavares punde tu baada ya mchezo huo. “Ukitazama katika mchezo huu (dhidi ya Mtibwa) wamefunga mabao mawili lakini walikuwa na uwezo wa kufunga mabao mengine manne, walikuwa bora,” aliongeza.

“Ukiniambia nifananishe na timu nyingine siwezi kusema sana lakini Simba wametulia, wanacheza kwa kutengeneza nafasi, ukiwa kama kocha nawe utapenda kuona timu yako inacheza vizuri.”