Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga muziki mnene

Muktasari:

Joshua anatumia nguvu na haogopi, Manyama anatumia akili, wakati Amos ana kasi.Mabeki wa kati ni Kelvin Yondani ‘Vidic’ na Nadir Haroub ‘Cannavaro’.

YANGA iliyokuwa kambini Zanzibar inarejea Dar es Salaam leo Alhamisi na inatarajiwa kuonekana kwa mara ya kwanza uwanjani wikiendi hii itakaposhuka kukipiga kwenye mchezo wa kirafiki ambao hata hivyo bado haujjathibitishwa.

Vijana hao wa Jangwani hawajacheza mechi yoyote Dar es Salaam tangu kuanza maandalizi ya msimu mpya wala mashabiki mji huo hawajakiona kikosi kipya chini ya Mbrazili Marcio Maximo.

Yanga ikiwa Zanzibar ilicheza mechi tatu za kirafiki dhidi ya Chipukizi ya Pemba, Shangani na KMKM za Unguja.

Maximo licha ya kusisitiza kwamba hajajua ni timu gani atacheza nayo, alisema anatarajia kupanga kikosi kamili kitakachocheza dakika zote 90 na kama atafanya mabadiliko, yatakuwa madogomadogo ya kawaida na tofauti kabisa na alivyokuwa anafanya kwenye mechi zake za kirafiki alizocheza Zanzibar ambapo kila mchezaji alicheza dakika 45.

“Mwanzo ulikuwa mgumu sana kwa wachezaji wangu kwani walikuwa na kazi ya kujifunza staili mpya za namna ninavyotaka wacheze, namna ya kumili mpira ninavyotaka, pasi za kueleweka kuchanganya na siyo kubutua bila mpango, kazi ambayo kwa sasa inakwenda vizuri.”

Uchunguzi uliofanywa na Mwanaspoti kulingana na mazoezi yake na mechi za kirafiki ‘First Eleven’ ya Maximo ni hii; Kipa ni Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul beki ya kulia na kushoto ni Oscar Joshua lakini Edward Manyama na Amos Abeil anaocheza nao nafasi moja ni hatari, Maximo anaweza kubadilika kulingana na wapinzani wake na walizonazo wachezaji hao.

Joshua anatumia nguvu na haogopi, Manyama anatumia akili, wakati Amos ana kasi.Mabeki wa kati ni Kelvin Yondani ‘Vidic’ na Nadir Haroub ‘Cannavaro’.

Kiungo mkabaji ni Mnyarwanda Mbuyu Twite na kiungo mshambuliaji ni Hassan Dilunga.

Panga pangua Mbrazili Andrey Coutinho atacheza winga ya kushoto na Mnyarwanda Haruna Niyonzima atacheza winga ya kulia, mastraika wa kati Mrisho Ngassa anayecheza kama kiungo nyuma ya Genilson Santos ‘Jaja’.

Simon Msuva anaweza kucheza winga ya kulia kama anataka timu ishambulie kwa kasi, Jerry Tegete, Hamis Kiiza raia wa Uganda, Said Bahanuzi na Hussein Javu nao wanaweza kumpeleka Ngassa pembeni.

Maximo atakuwa na mpango wa kucheza mpira wa kutulia.

Mashabiki wa Wana Jangwani hao wanaisubiri kwa hamu timu hiyo ili kuona makali ya vifaa vipya.