Yanga, Mtibwa shughuli bado ngumu kwa Mkapa!

Mashabiki wa Yanga wanasubiri kipindi cha pili kuona kama kitawapa kicheko baada ya dakika 45 za kwanza kumalizika bila kufungana na Mtibwa Sugar ya Morogoro.

Mechi ilianza kwa kasi kwa Yanga ambapo wachezaji walipambana kutaka bao la mapema kabla ya Mtibwa Sugar kuanza kucheza kwa kupaki basi.

Mwanaspoti linakuchambulia jinsi mchezo ilivyokuwa hadi kipindi cha kwanza kukosekana mbabe

MOTO WA YANGA NDANI YA DAKIKA 5

Yanga ilianza kwa kasi kubwa katika dakika tano za mwanzo ambapo safu yake ya mbele iliichachafya ngome ya ulinzi ya Mtibwa Sugar. 

Dakika ya pili ilitokea piga nipige katika eneo la golikipa wa Mtibwa Sugar, Abuutwalib Mshery ambapo mabeki wake walikuwa na presha ya kuokoa hatari,lakini kipa akauchomoa mpira katikati ya miguu yao.

Kasi ya Yanga nikama imewapa akili Mtibwa Sugar kuanza dakika ya saba, kurudi nyuma na kwenda kushambulia kwa kushitukiza.

Kutokana muda mwingi kupaki  basi.

Plani yao iliwawia vigumu kufika langoni kwa Yanga na kinda Shikalo asiwe na presha, tofauti na kipa wa Mtibwa Sugar alikutana na kashikashi za Ditram Nchimbi, Tuisila Kisinda na Deus Kaseke waliokuwa wanafika zaidi langoni kwake.

DAKIKA YA 30

Mtibwa Sugar ilianza kucheza maeneo yote ya uwanja kwa maana ya kuruhusu kucheza kuanzia kwa kipa, kati na mbele.

Kitendo cha Mtibwa Sugar kucheza kwa kujiamini kiliibua ushindani wa kila timu kuanza kusaka  bao.

Yanga haukuwa nyuma pamoja na Mtibwa Sugar kuonekana kujibizana nao kwa kushambuliana imeendelea kufika mara nyingi langoni kwa mpinzani wake.

Dakika ya 35  Fei Toto alijaribu kupiga shuti  kali karibia na 18 ya Mtibwa Sugar, kipa Mshery aliipangua kwa mkono akaitoa nje.

Yanga iliendelea kumiliki mpira ambapo Kaseke alimchongea pasi nzuri Fei Toto akapiga mpira ambao ulipaa juu.

Kikosi cha Yanga ni Faruk Shikalo, Kibwana Shomari, Yassin Mustapha, Lamine Moro, Bakari Mwamnyeto, Mukoko Tonombe, Ditram Nchimbi, Feisal Salum, Michael Sarpong, Deus Kaseke na Tuisila Kusinda.

Walio benchi ni Metacha Mnata, Said Juma, Zawadi Mauya, Carlos, Fiston Abdul na Tuisila Kisinda.

Kikosi cha Mtibwa Sugar, Abuutwalib Mshery, Hassan Ramadhan, Issa Rashid, Geoffrey Kigi, Dickson Mbeikya, Baraka Majogoro, Ally Yusuph, Kassim Hamis, Kelvin Kongwe, Riphat Msuya na George Makanga.

Waliopo benchi ni Shaaban Kado, Salum Kanoni, Jamal Masenga,Juma Ganambali, Awadhi Juma, Harun Chanongo na Ismail Mhesa.