Anapasuka mtu mapemaaa!

Saturday February 20 2021
Hitimana pic
By Waandishi Wetu

KUNA dakika 270 leo katika viwanja vitatu tofauti zikiwa ni mechi tatu za Ligi Kuu Bara zitapigwa na timu zote sita zinawania pointi tatu muhimu na kila moja ikiwa na malengo yake.

Ihefu wakiwa wameanza kuzinduka watakuwa nyumbani wakiwakaribisha Mwadui ya Shinyanga ambayo inapambana na roho yake ikiwa imezibeba timu zote 17 juu yao, lakini pia Uwanja wa Uhuru wenyeji KMC wata-pambana na Kagera Sugar katika mchezo wa mapema lakini mechi kubwa itakuwa baadaye usiku wakati Yanga wakiikabili Mtibwa Sugar.

Yanga vs Mtibwa

Yanga watakuwa na vita na Mtibwa ambao ni ndugu wa Kagera ambao almanusu-ra wawatibulie rekodi yao ya kutofungwa katika ligi, katika mchezo uliopigwa katikati ya wiki hii wakichomoa na mchezo kumalizika 3-3 matokeo ambayo yalizusha tafrani nyingi nna vikao virefu vyenye swali moja tu kulikoni haya yanatokea.

Mchezo huu utakuwa ni kama vita ya Kirundi kutokana na vikosi vyote kufundishwa na majkocha kutoka Burundi tena wanaojuana lakini pia wanaopenda soka la pasi za kutosha vita ambayo itaongeza ugumu wa mchezo huo ambapo sasa ni ubora wa mbinu na wachezaji kujiongeza ndio utakaotoa matokeo kwa mshindi.

Yanga haijashinda mechi zake tatu zilizopita katika ligi wakiambulia pointi tatu baada ya sare tatu matokeo ambayo yameanza kutishia mbio zao za kutamani kuwa mabingwa msimu huu huku hatua mbaya zaidi ni kwamba watani wao Simba ambao muda mrefu wame-kuwa nyuma yao wanaendelea kushinda mechi zao za viporo na kama wakishinda zote mbili basi Yanga itaondolewa juu ya msimamo huo.

Advertisement

Hatua hiyo ndio iliyowafanya mabosi wa Yanga mara baada ya mchezo wao wa Kagera kukesha usiku kucha na kikosi chao kwa vikao virefu vya kuhakikisha hali inarejea katika utulivu wakijua wazi kwamba mbali na malengo yao wanakutana na Mtibwa ambao huwa hawatabiriki.

Vikao hivyo Mwanaspoti limejulishwa kwamba mambo yako sawa sasa na wachezaji mpaka makocha akili yao ni katika vita ya Mtibwa kuhakikisha wanawarejeshea tabasamu mashabiki wao ambao walikuwa wakali katikati ya wiki kiasi cha kutamani kuwararua viongozi wao.

Kazi kubwa katika siku ya juzi na jana katika maz-oezi ya Yanga chini ya kocha wao Cedric Kaze imekuwa kwanza kurudisha saikolojia ya ushindi kwa wachezaji wake lakini pili amekuwa akikomaa na safu ya ulinzi yao ambayo imekuwa ikifanya makosa

.Kinachowapasua makocha wa Yanga ni hatua ya timu yao kuruhusu bao kila mchezo uliopita huku lakini mbaya ni kwamba mchezo wa Kagera mabeki wao wakaruhusu mabao matatu katika mechi moja yakiwa ndio mabao mengi kuruhusu msimu huu katika mchezo mmoja.

Mbali na mazoezi hayo ya safu ya ulinzi pia Kaze amekuwa akikomaa na jinsi ya kutengeneza nafasi na ku-malizia kwa urahisi ambapo kwa mazoezi ya jana apana shaka kunaweza kwua na mabadiliko karibu kila idara ya timu hiyo katika mchezo wa leo.

Kiungo wa Yanga Mukoko Tonombe alisema; “Tunakwenda kucheza na Mtibwa Sugar ni mechi ngumu lakini hii mechi im-ekuja wakati ambao lazima tupate matokeo baada ya kushindwa kushinda mechi zilizopita, hii ni mechi ya kurudisha utulivu kwenye timu yetu, tumekubaliana hivyo kama wachezaji jambo zuri makocha wamekuwa wakitupa mbinu ya kuondoa makosa ambayo tulikuwa tumeyafanya.

”Mtibwa wao hawawacheki sana Yanga kwani nao wametoka kuzuiwa nyumbani tena wakisawazisha bao katika mchezo dhidi ya Ihefu na sasa wanatamani kutafuta ushindi wa kwanza katika ligi tangu mwaka 2021 uanze.

Ikiwa chini ya kocha Thienry Hitimana Mtibwa ambao wanaoshikilia nafasi ya 11 katika msimamo watataka kuhakikisha wanarejesha kama sio kuiongeza maumivu katika kidonda cha Yanga kilichotengenezwa na ndugu zao Kagera akijivunia kurejea kwa mshambuliaji wao Kelvin Kongwe ambaye ndiye aliyewaokoa katika mchezo dhidi ya Ihefu.

Akizungumza na Mwanaspoti Hitimana alisema: “Mchezo ujao na Yanga utakuwa mgumu na wenye ushindani sana, sisi tunahitaji matokeo na Yanga wanahitaji pia matokeo hivyo na wote tumetoka kuambulia pointi moja ila tunasubiri dakika 90 zitasema lakini bora tupate pointi moja kuliko kukosa.”Hitimana alisema, Yanga ina wachezaji wa kimataifa ambao wana uwezo mkubwa hivyo vijana wake wana-takiwa kuwa makini na kujiamini katika mchezo huo.

Kuelekea mchezo huo amesema kuna wache-zaji wake wawili Baraka Ma-jogoro na Salum Kihimbwa waliopata majeraha katika katika mchezo uliopita.
Advertisement