Kaze amrudisha Shikhalo, apanga silaha mpya kiwavaa Mtibwa

Saturday February 20 2021
shikalo pic

WAKATI Yanga ikibakiza masaa machache kuingia uwanjani kupambana na Mtibwa Sugar kocha wa timu hiyo Cedric Kaze amefanya mabadiliko mabadiliko manne katika kikosi chake.

Anzia katika ukuta Kaze amerudisha kipa Mkenya Farouk Shikhalo langoni akipishana na Metacha Mnata ambaye ndio kipa aliyecheza mechi nyingi.

Hii ni mechi ya pili katika ligi kwa Shikhalo ambaye alicheza mechi moja pekee ya ligi msimu huu kabla ya leo alipofungua pazia la ligi dhidi ya Prisons kisha baadaye kuumia.

Hata hivyo kipa huyo Mkenya ndiye aliyesimama langoni katika mechi zote wakati Yanga ikichukua Kombe la Mapinduzi Kisiwani Zanzibar huku Shikhalo akiwa ndio shujaa wa timu hiyo akionyesha uwezo mkubwa.

Hakuna mabadiliko katika mabeki wote akiirudisha safu ile ile ya kulia akiwa Kibwana Shomari,kushoto Mustapha Yassin wakati mabeki wa kati wakiendelea manahodha Lamine Moro na msaidizi wake Bakari Mwamnyeto.

Safu ya kiungo Mukoko Tonombe ambaye mchezo wa kwanza alianzia benchi akiingia kipindo cha pili,leo amerudishwa katika kikosi kinachoanza akicheza sambamba na Feisal Salum,Tuisila Kisinda na Ditram Nchimbi ambaye ameanza pia.

Advertisement

Kuanza kwa Mukoko kunamfanya Zawadi Mauya kurudi benchi huku pia Nchimbi akichukua nafasi ya Farid Mussa ambaye alianza katika benchi ingawa leo ameanzia benchi.

Safu ya ushambuliaji Kaze ameendelea kuamiani Michael Sarpong aliyepika bao moja katika sare ya mabao 3-3 dhidi ya Kagera Sugar akicheza sambamba na Deuse Kaseke aliyefunga bao hilo.

Kwenye benchi Kaze amewapa nafasi Mnata,mabeki Said Makapu,Adeyum Saleh,viungo Zwadi Mauya,Carlos Guimaraes 'Carlinhos',Farid Mussa na mshambuliaji Fiston Abdulrazack

Advertisement