Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yahya aahidi mabao zaidi Azam

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Azam, Yahya Mohammed amesema dhamira yake ni kufunga mabao mengi yatakayoiwezesha Azam kushika nafasi za juu katika Ligi Kuu.

Mghana huyo ameanza vizuri msimu wa Ligi Kuu kwa kufunga bao pekee lililoiwezesha Azam kuibwaga Ndanda kwa bao 1-0 katika mechi ya ufunguzi iliyochezwa katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona Mkoani Mtwara.

Yahya alisema ni jambo la faraja kufunga bao muhimu kwa timu yake katika uwanja wa ugenini.

“Ni mwanzo mzuri kwa timu na muhimu ni kupata matokeo, nimefurahi kufunga na ninaamini nitakuwa na msimu mzuri hapa. Nahitaji kushinda mataji na Azam,”alisema Mohammed aliyesajiliwa kutoka Adouna Stars ya Ghana.

Akizungumzia mechi inayofuata dhidi ya Simba, Mohammed alikiri utakuwa mgumu, lakini wamejiandaa kukabiliana nayo.

“Tutatumia kipindi cha mapumziko kujiandaa, Simba ni timu nzuri yenye wachezaji wazoefu na wengine walikuwa Azam, tunajuana vizuri lakini kwenye kila mmoja atakuwa na kazi ya kuisaidia timu yake,”alieleza.

Wachezaji walioihama Azam na kujiunga na Simba ni John Bocco, Aishi Manula, Shomari Kapombe na Erasto Nyoni.

Wakati huohuo kikosi cha Azam kitaingia kambini kesho kujiandaa na mechi dhidi ya Simba bila kuwa na wachezaji wawili, Himid Mao na Mwadin Ally ambao wameitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars kinachojiandaa na mechi ya kirafiki dhidi ya Botswana.