Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yacouba, Kambole ndani Mapinduzi

WACHEZAJI 25 wa kikosi cha Yanga wamewasiri tayari kwaajili ya mashindano ya Mapinduzi huku mastaa wao wote wa kikosi cha kwanza wakiachwa Dar es Salaam.

Kikosi hicho kikiongozwa na Kocha msaidizi Cedrick Kaze ambaye ameongozana na mastaa wa kikosi cha kwanza nahodha Bakari Mwamnyeto na Farid Mussa kitakuwa na mchezo kesho kutwa dhidi ya KMKM.

Mastaa wengine wa kikosi cha Yanga ni Zawadi Mauya, Gael Bigirimana, Crispin Ngushi, Dickson Ambundo, Clement Mziza, David Bryson, Ibrahim Abdallah ‘Bacca’ Abdallah Shaibu Ninja na Kipa Erick Johora.

Wachezaji wa zamani wa Yanga ambao wapo kwenye mchakato wa kuingizwa kwenye usajili mpya ndani ya timu hiyo Lazarous Kambole na Yacouba Sogne ni miongoni mwa mastaa waliokuja kushiriki Mapinduzi.

Wachezaji walioongezwa kikosini kutoka timu ya vijana ni makipa Hajji Mohammed Abassi, Jacob Timoth Ipwaya, mabeki Maulid Kiakala, Ally Said Mohammed na Mohammed Omary.

Wakati viungo ni Arafat Hussein, Ahmed Fred, Maulid Timoth na eneo la ushambuliaji ni Nasri Ally, Rymond Ntaudyimara, Daruwesh Rashid na Shaibu Shaibu Mtita.