Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chama la Wana, Geita kumaliza ubishi

Muktasari:

  • Timu hizo zinakutana baada ya mechi ya kwanza iliyopigwa Uwanja wa Nyankumbu, mjini Geita kumlizika kwa sare ya mabao 2-2, hali inayoongeza mvuto wa kusubiria ni nani atakayeibuka kidedea kutokana na ushindani baina ya miamba hiyo miwili.

MECHI ya marudiano ya play-off kusaka tiketi ya kucheza Ligi Kuu Bara msimu ujao, inapigwa leo ambapo wenyeji, Stand United ‘Chama la Wana’, itakuwa kwenye Uwanja wa Kambarage, mjini Shinyanga kumalizana na Geita Gold.

Timu hizo zinakutana baada ya mechi ya kwanza iliyopigwa Uwanja wa Nyankumbu, mjini Geita kumlizika kwa sare ya mabao 2-2, hali inayoongeza mvuto wa kusubiria ni nani atakayeibuka kidedea kutokana na ushindani baina ya miamba hiyo miwili.

Stand United imemaliza nafasi ya tatu na pointi pointi 61, huku Geita Gold ikimaliza ya nne na pointi 56 na kuhitimisha timu mbili za kuchuana play-off, baada ya Mtibwa Sugar na Mbeya City kupanda Ligi Kuu Bara moja kwa moja msimu ujao.

Mtibwa iliyoshuka daraja msimu uliopita, imerejea tena baada ya kuongoza Ligi ya Championship na pointi 71, huku Mbeya City iliyoporomoka msimu wa 2022-2023, ikirejea kwam kushika nafasi ya pili na pointi 68.

Stand iliyoshuka daraja msimu wa 2018-2019, katika mechi tatu za msimu huu haijashinda kwa Geita Gold, kwani ya kwanza kukutana ilichapwa ugenini mabao 3-1, Januari 12, 2025, huku marudiano zilipokutana zilitoka sare ya 1-1, Mei 11, 2025.

Katika mechi ya tatu ambayo ilikuwa ya play off iliyopigwa Mei 24, 2025, timu hizo zikatoka sare ya 2-2, kitu kinachosubiriwa kuona na leo ni kipi kitakachojiri, ikiwa ni dakika 90 za mbivu na mbichi baina ya miamba hiyo.

Akizungumza na Mwanaspoti, nyota wa Stand United, Lucas Sendama alisema licha ya sare waliyoipata ugenini, wanatambua ugumu uliopo, japo imewapa nguvu na motisha ya kupambana ili kutimiza malengo ya kukirejesha kikosi hicho Ligi Kuu Bara.

Kwa upande wa mshambuliaji wa Geita Gold, Andrew Simchimba alisema wanaingia katika mechi hiyo muhimu na ya uamuzi kwao kabla ya hatua ya mwisho, hivyo wao kama wachezaji watapambana ili kufanikisha hilo, licha ya ushindani uliopo mbeleni.

Stand United itaendelea kuwategemea nyota wawili muhimu wa timu hiyo katika eneo la ushambuliaji, ambao ni Omary Issa ‘Berbatov’ aliyemaliza msimu huu akiwa na mabao tisa, akifuatiwa na mchezaji mwenzake, Emmanuel Manyanda mwenye manane.

Kwa upande wa Geita inaingia katika mechi hii ikimtegemea mshambuliaji nyota na kinara wa mabao wa Ligi ya Championship msimu huu Andrew Simchimba aliyefunga mabao 18 sawa na Raizin Hafidh wa Mtibwa Sugar na Abdulaziz Shahame wa TMA Stars.

Mshindi wa jumla wa mechi hii atapata nafasi ya kuvaana na timu inatakayopoteza play off ya zile za Ligi Kuu inayozikutanisha itakayoshika nafasi ya 13 na 14 zitakazocheza zenyewe ili kutafuta kubaki kwa msimu ujao au iungane na KenGold na Kagera Sugar zilizoshuka daraja mapema.