Yacouba awanyanyua Yanga

Muktasari:
Kwa mara nyingine tena leo, Mshambuliaji Yacouba Songne amefanikiwa kuwanyanyua mashabiki wa Yanga kwa kuandika bao la kuongoza dhidi ya JKT Tanzania.
Kwa mara nyingine tena leo, Mshambuliaji Yacouba Songne amefanikiwa kuwanyanyua mashabiki wa Yanga kwa kuandika bao la kuongoza dhidi ya JKT Tanzania.
Baada ya kufunga bao lililokataliwa kwenye mchezo uliopita dhidi ya Namungo, leo tena Songne amewanyanyua wananchi hao kwa bao safi la kichwa maridadi kilichomuacha kipa, Joseph Ilunda akiwa amesimama.

Bao hilo limetokea wakati ambao Yanga ilikuwa inafanya mashambulizi makali langoni mwa maafande JKT Tanzania.
Mabeki JKT wampa bao tamu Kisinda
Kosa la mabeki wa JKT Tanzania kuzembea na mpira umemfanya winga machachari wa Yanga, Tuisila Kisinda afunge bao tamu kwa timu yake na kuifanya kuongoza 2-0.
Kuchanganyana kwa mabeki wanaoongozwa na David Mwantika, kugongana na mpira uliomfikia Kisinda, aliyeujaza pembeni mwa kipa Joseph Ilunda kumuacha amesimama.

Bao hilo ni la pili kwa Yanga ambao tangu mwanzo mwa mchezo, walionekana kusaka mabao ya mapema jambo ambalo wamefanikiwa.
Licha ya maafande JKT kujaribu kucheza, jitihada zao zimeshindwa kabisa kufua dafu mbele ya Yanga ambao wamecheza vema zaidi dakika 30 za mwanzo wa mchezo huu.
Imeandikwa na Matereka Jalilu