Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wibol Maseke aomba msimu uishe tu

MASEKE Pict

Muktasari:

  • Maseke ametumika katika mechi sita za Ligi Kuu Bara na moja ya Kombe la Shirikisho (FA), huku muda mwingi akiishia kukaa benchi kitu ambacho kimemkosesha raha na kuona hana namna ila kujipanga upya kwa msimu ujao baada ya msimu huu kumkataa.

KIPA wa KMC, Wibol Maseke amesema kwa namna mambo yalivyomuendea kombo akiwa na kikosi hicho kwa msimu huu kwa kucheza mechi saba tu, anaona ni vyema msimu ulishe ili ajipange upya.

Maseke ametumika katika mechi sita za Ligi Kuu Bara na moja ya Kombe la Shirikisho (FA), huku muda mwingi akiishia kukaa benchi kitu ambacho kimemkosesha raha na kuona hana namna ila kujipanga upya kwa msimu ujao baada ya msimu huu kumkataa.

Kipa huyo wa zamani wa Azam, amedaka mechi za Ligi Kuu dhidi ya Namungo (nyumbani), Dodoma Jiji (ugenini), Mashujaa FC (nyumbani), Pamba FC (nyumbani), Tabora United (nyumbani) na ile ya JKT Tanzania na alijifunga bao.

Akizungumza na Mwanaspoti, Maseke alisema mbali na ushindani wa namba uliopo katika nafasi anayocheza, lakini kuna changamoto za nje ya kazi ambazo zimechangia kwa kiasi kikubwa kucheza mechi chache hata hivyo hakusema nini kinamsumbua.

"Ni kawaida katika soka mchezaji kucheza kwa mafanikio na wakati mwingine kushuka kiwango, kikubwa ni kutokukata tamaa, maana ni kazi yetu, lazima kuendeleza mapambano, ndiyo maana najipanga kwa msimu ujao," alisema Maseke na kuongeza;  

"Siwezi kusema nina matarajio makubwa katika mechi tatu zilizosalia dhidi ya Tabora, Mashujaa na Pamba Jiji, maana ndiyo tunaelekea kumaliza msimu."

Maseke ameweka rekodi ya kuwa kipa wa kwanza kujifunga katika misimu miwili mfululizo, kwani msimu uliopita alijifunga dhidi ya Tanzania Prisons kabla ya msimu huu kujiweka katika kipigo cha mabao 2-0 mbele ya maafande wa JKT Tanzania mechi iliyokuwa ya mwisho kuonekana uwanjani.

Mbali na hilo aliwataja makipa waliyofanya vizuri kwa upande msimu huu ni Moussa Camara na  Castor Mhagama wa KenGold, huku akimtabiria Prince Dube wa Yanga kustahili kupewa Tuzo ya Mchezaji Bora kwa kiwango alichokionyesha cha kufunga mabao akiwa na 12 kama Jean Ahoua wa Simba.