Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wepesi tu! watatulia

Muktasari:

  • Ndio! Kwani wewe ni nani hadi usiishingilie Yanga wakati hao Simba wenyewe kimoyomoyo wanataka Yanga iwachape tena za kutosha tu hao Welaytta Dicha kutoka Ethiopia ili kupeperusha vyema bendera ya Tanzania.

WAKATI kule England shughuli zitasimama ili mashabiki kushuhudia mtanange wa Manchester Derby, hapa nyumbani Tanzania mambo yote yatakuwa pale Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kushangilia Yanga tu.

Ndio! Kwani wewe ni nani hadi usiishingilie Yanga wakati hao Simba wenyewe kimoyomoyo wanataka Yanga iwachape tena za kutosha tu hao Welaytta Dicha kutoka Ethiopia ili kupeperusha vyema bendera ya Tanzania.

Lakini, Yanga itaingia uwanjani bila mastaa wake wanne wa kikosi cha kwanza, hata hivyo hilo halijawahi kuwa tatizo kabisa kwa kocha, George Lwandamina.

Iko hivi. Straika tegemeo kwa sasa klabuni hapo, Obrey Chirwa atakuwa jukwaa kutokana na kutumikia adhabu, lakini Lwandamina na mashabiki wa Yanga, wamewatazama Ibrahim Ajibu na Pius Buswita kisha wakasema wanatosha kuwamaliza Welaytta mapema tu.

Yanga na Wahabeshi wanakutana kwenye mchezo wa raundi ya kwanza kuwania kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambapo Yanga inahitaji ushindi nyumbani ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kusonga mbele.

Hata hivyo, hofu kubwa ya Yanga ilikuwa ni kuwakosa Chirwa, Kelvin Yondani na Papy Tshishimbi, ila uwepo wa Ajibu na Buswita ambao wamefunga mabao 11 kwa pamoja Ligi Kuu Bara msimu huu, umewapa mzuka kinoma.

Kutokana na uzito wa mchezo huo, Yanga iliweka kambi ya siku nne kule Morogoro kwa kukisuka upya kikosi chake chini ya Lwandamina.

Lakini, wakati mastaa hao wanne wakikosekana kwenye mchezo huo, straika wa Zimbabwe Donald Ngoma, ambaye alipewa majukumu ya kuongoza jahazi la Yanga, hatakuwemo pia.

Katika kambi yake kule Morogoro, Lwandamina alitumia muda mwingi kumnoa Ngoma ili kuwa na makali, lakini habari mbaya ni kuwa Ngoma hatacheza baada ya kujitonesha jaraha lake tena akiwa mazoezini.

Kocha msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa ‘Fusso’, ambaye amepona kiaina na kibano cha kufungiwa katika mchezo wa leo kisha majanga kumuangukia Mzambia, Noel Mwandila alisema wamekamilisha maandalizi yao.

Pia, alisema wameichunguza vya kutosha Dicha na kubaini ubora na upungufu wa kikosi chake.

“Tumemaliza kambi yetu, viongozi walituwezesha kupata taarifa za wapinzani wetu na tumewasoma na kuwaelekeza vijana wetu yote ya kufanyika uwanjani.

“Tutawakosa Ngoma na Amissi Tambwe ambao walipata matatizo ya ghafla siku ya misho ya kambi yetu, lakini tayari tumepata watu wa kuziba nafasi zao na kila kitu kitakwenda vizuri,” alisema Nsajigwa.

DICHA WANENA

Kocha wa Dicha, Ato Zenebe Fisseha alisema wanaiheshimu Yanga kwa kuwa ni timu kongwe, lakini wamekuja kupambana nao kutafuta tiketi ya kutinga hatua ya makundi.

Alisema Dicha ni timu changa na kamwe hawawezi kujilinganisha na Yanga, lakini wanataka kuweka historia kwa kufika mbali katika mashindano hayo ingawa wanatambua changamoto zake.

“Tumekuja kupambana, tunaiheshimu sana Yanga na ukiwa Ethiopia utaambiwa ni timu kubwa na kongwe wanaiheshimu sana, lakini hatutaki kuogopa jina lao, tunachotaka ni kupambana nao tuweke historia,” alisema.