Wasifu wa CEO mpya Simba huu hapa...
LEO Januari 26, 2022 Simba imemtangaza Imani Kajula kuwa Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa klabu hiyo aliyechukua nafasi ya Mwanamama Barbara Gonzalez aliyejiuzulu Disemba 10 mwaka jana.
Kajula ambaye ni mwanachama wa muda mrefu wa Simba ni mbobezi katika masuala ya Kibenki na masoko akiwa na uzoefu wa kutosha aliouvuna akihudumu katika taasisi mbalimbali.
Pia ni mzoefu kwenye masuala ya uongozi wa mpira kwani alikuwepo kwenye Kamati ya Maandalizi ya Michuano ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 (AFCON U17) iliyofanyika nchini mwaka 2019.
Akiwa Mkurugenzi wa kampuni ya mawasiliano na masoko ya EAG Group Kajula alikuwa sehemu ya maandalizi ya Wiki ya Simba mpaka kilele chake (Simba Day) mwaka jana ambapo kampuni hiyo ndiyo ilitengeneza mitandao ya kijamii ya klabu hiyo.
Mwaka 1999 hadi 2003, Kajula alikuwa Meneja masoko wa banki ya CRDB, na mwaka 2003 hadi 2006 akawa Mkurugenzi wa masoko na Biashara katika benki ya Posta Tanzania (TPB), na 2006 hadi 2013 akawa mkuu waq Masoko na Mawasiliano wa NMB.
Hadi sasa wakati Simba inamchagua kuwa CEO wake alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa EAG Group aliyoingoza tangu mwaka 2013