Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pamba Jiji yatua kwa beki Mzambia

PAMBA Pict

Muktasari:

  • Taarifa kutoka timu hiyo, zimeliambia Mwanaspoti wawakilishi hao wametua Zambia tayari kwa kufanikisha dili la aliyekuwa kiungo nyota wa Simba, Larry Bwalya anayeichezea Napsa Stars FC, ingawa wanaangalia pia na upatikanaji wa Kabaso Chongo.

MABOSI wa Pamba Jiji wameanza harakati mapema za kukisuka kikosi hicho upya ili kuleta ushindani msimu ujao, ambapo inaelezwa wametuma wawakilishi kufuatilia upatikanaji wa beki wa kati wa Kabwe Warriors ya Zambia, Kabaso Chongo.

Taarifa kutoka timu hiyo, zimeliambia Mwanaspoti wawakilishi hao wametua Zambia tayari kwa kufanikisha dili la aliyekuwa kiungo nyota wa Simba, Larry Bwalya anayeichezea Napsa Stars FC, ingawa wanaangalia pia na upatikanaji wa Kabaso Chongo.

Mmoja wa kiongozi wa timu hiyo, aliliambia Mwanaspoti wanataka kukamilisha dili hizo zote mbili wakiwa Zambia, japo moja ya changamoto zilizopo ni kiasi kikubwa cha mastaa hao wanachokihitaji, ingawa wanaendelea kupambana kama watafanikiwa.

“Mazungumzo yanaenda vizuri na tunashukuru hata Bwalya amekubali kupunguza kiasi cha fedha tofauti na kile alichohitaji mwanzo, ingawa dili halijakamilika, tunaangalia uwezekano pia kama tutavunja mkataba wa Kabaso,” kilisema chanzo hicho.

Kwa upande wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Pamba, Peter Juma Lehhet, alisema baada ya msimu kuisha na kikosi hicho kunusurika kushuka daraja, kwa sasa wanajipanga ili kufanya usajili wa nguvu, utakaoleta tija na kuleta ushindani kwa msimu ujao.

“Masuala yote yanayohusu usajili naomba unipe muda kidogo kwa sababu ushindani ni mkubwa kutokana na mahitaji ya kila timu, hivyo, ni lazima tujipange kwa kuangalia namna nzuri pia ya kukabiliana na washindani wetu sokoni,” alisema.

Mwanaspoti linatambua, Bwalya amemaliza mkataba na Napsa Stars, huku akizichezea Simba ya Tanzania, Dynamos ya Zambia, AmaZulu na Sekhukhune United za Afrika ya Kusini na sasa, imebaki kukubaliana maslahi binafsi tu.

Kwa upande wa Kabaso anayecheza beki wa kulia, beki wa kati na kiungo mkabaji kwa ufasaha, alijiunga na Kabwe Warriors, Julai 2, 2024, akitokea TP Mazembe ya DR Congo, ambako mkataba wake na kikosi hicho unafikia mwisho, Desemba 31, 2025.

Kabaso aliyezaliwa Februari 11, 1992, akiwa na miaka 33, ameiwezesha Kabwe Warriors kumaliza Ligi Kuu ya Zambia msimu wa 2024-25, ikiwa nafasi ya tano kwa pointi 51, ikishinda mechi 13, sare 12 na kupoteza tisa kati ya 34, iliyocheza.

Pamba iliyorejea Ligi Kuu Bara msimu wa 2024-2025, baada ya miaka 23 tangu iliposhuka daraja mwaka 2001, imemaliza msimu ikiwa nafasi ya 11 kwa kuwa na pointi 34, ikishinda mechi nane, sare 10 na kupoteza 12, kati ya 30, ikifunga mabao 22 na kuruhusu 33.