Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtanzania mwingine kucheza UEFA

UEFA Pict

Muktasari:

  • Floriana FC inashiriki Ligi Kuu ya Malta, maarufu kama Maltese Premier League, ambayo ni ligi ya daraja la juu katika mfumo wa soka nchini humo. Malta ni nchi ndogo ya visiwa iliyoko katika Bahari ya Mediterania kati ya Italia na Afrika Kaskazini.

TANZANIA itaendelea kuwakilishwa na nyota mwingine kwenye michuano ya Ulaya, kiungo Charles M’Mombwa ambaye hivi karibuni alijiunga na Floriana FC ya Malta.

Floriana FC inashiriki Ligi Kuu ya Malta, maarufu kama Maltese Premier League, ambayo ni ligi ya daraja la juu katika mfumo wa soka nchini humo. Malta ni nchi ndogo ya visiwa iliyoko katika Bahari ya Mediterania kati ya Italia na Afrika Kaskazini.

M’Mombwa (27) alijiunga na klabu hiyo akitokea Newcastle Jets ya Ligi Kuu Australia na anakuwa Mtanzania wa tatu katika historia kushiriki michuano ya UEFA, akifuata nyayo za Mbwana Samatta na Novatus Miroshi.

Samatta aliandika historia ya kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza UEFA Champions League akiwa na KRC Genk, huku Miroshi akicheza mechi za Europa Conference League akiwa na Shakhtar Donetsk.

Iko hivi, klabu ya Mtanzania huyo ilimaliza katika nafasi ya tatu kwenye ligi ya Malta, hivyo itashiriki UEFA Europa Conference League itakayoanza mwezi ujao.

Kwenye hatua ya mtoano (First Qualifying Round), klabu hiyo itaanza dhidi ya Haverfordwest County ya Wales Julai 5, kabla ya kurudiana Julai 17.

Kama atapata nafasi ya kucheza katika michuano hiyo, itakuwa ni mara ya kwanza kwa M’Mombwa kushiriki mashindano ya UEFA, kwani hapo kabla alikuwa anawaangalia Samatta na Novatus kwenye televisheni.

“Tunamkaribisha Charles kwenye familia yetu. Tunaamini uzoefu wake kwenye ligi kubwa kama Australia na mechi za kimataifa na Taifa Stars utakuwa msaada mkubwa kwa kikosi chetu,” ilisomeka taarifa ya utambulisho wake.

Akiwa Newcastle Jets, kiungo huyo alicheza mechi 13 kwa dakika 498 na kufunga bao moja.