Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanne Yanga wapewa Coastal Union

WACHEZAJI wanne wa Yanga, Aboutwalib Msheri, Farid Mussa, Jesus Moloko na Chico Ushindi wamepewa nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha Yanga kitakachoingia Uwanja wa Benjamin Mkapa, usiku wa leo kucheza na Coastal Union.

Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu itakayoanza saa 2:30 Usiku, ambayo Yanga inahitaji ushindi ili kutwaa ubingwa wa msimu huu, kocha Mkuu wa Yanga, Nassredine Nabi amewaanzisha nyota hao ambao hawakuanza kwenye mechi ya mwisho ya timu hiyo ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba ikishinda 1-0.

Mshery amechukua bafasi ya Djigui Diarra, Farid akiingia kwa Kibwana Shomari, huku Moloko na Ushindi wakichukua nafasi za Nahodha Bakari Mwamnyeto na Herritier Makambo.

Katika mechi ya leo, Msheri atakuwa golini na eneo la mabeki wataanza Djuma Shabani, Farid, Dickson Job na Yanick Bangala.

Eneo la kiungo Nabi amewaanzisha, Khalid Aucho, Feisal Salum, Salum Abubakar,  huku Moloko, Ushindi na Fiston Mayele wakipangwa kucheza mbele.

Benchi wapo Erick Johora, Paulo Godfrey, Yassin Mustapha, Ibrahim Bacca, Deus Kaseke, Dickson Ambundo, Denis Nkane, Chrispin Ngushi na Makambo.

Kama Yanga itashinda leo, itafikisha alama 67 na kuwa bingwa kwani hakuna timu nyingine kwa msimu huu itafikisha pointi hizo katika mechi zilizosalia.