Wanne waingia mitini uchaguzi wa TFF

Mgombea urais wa TFF, Hawa Mniga akiondoka baada ya kurudisha fomu katika ofisi za shirikisho hilo. Picha na Michael Matemanga
Muktasari:
ZOEZI la kuchukua na kurudisha fomu za kuwania nafai mbali mbali za uongozi ndani ya shirikisho la soka Tanzania limemalizika leo na wagombea wanne kati ya 10 waliochukua fomu za kuwania nafasi ya urais wameingia mitini.+
ZOEZI la kuchukua na kurudisha fomu za kuwania nafai mbali mbali za uongozi ndani ya shirikisho la soka Tanzania limemalizika leo na wagombea wanne kati ya 10 waliochukua fomu za kuwania nafasi ya urais wameingia mitini.
Kati ya wagombea hao 10 ni Ally Mayay Tembele, Ally Saleh, Evans G. Mgeusa, Hawa Mniga, Oscar Oscar na Wallace Karia ndio waliorudisha.
Wagombe ambao hawajarudisha fomu hadi taarifa ya Tff inatoka ni Deogratius Mutungi, Rahim Kangezi 'Zamunda' Zahor Mohammed Haji na Abbass Tarimba.
Kwa upande wa Kanda, kwenye kanda namba moja ya Dar es salaam, Morogoro, Mtwara na Pwani waliochukua na kurudisha ni pamoja na Athuman Kingome Kambi, Elisony Mweladzi, Jimmy Shomari Msindo, Lameck Nyambaya, Liston Katabazi, Saady Mohamed Khimji na Hosseah Lugano.
Kanda namba ya tatu ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Tanga waliochukua na kurudisha ni Khalid Abdallah Mohamed, Zakayo Mjema na Thabithy Kandoro.
Wakati kanda namba tatu ya Iringa, Mbeya, Njombe, Ruvuma na Songwe waliochukua na kurudisha ni Abousfian Sillia, James Mhagama, Joseph A. Ngunangwa, Ulisaja Elias, Denis Manumbu na Mohamed Mashango.
Kanda namba nne ya Dodoma, Shinyanga, Simiyu na Singida waliochukua na kurudisha ni Hamis Juma Kitila, Mohamed Aden, Osuri Kosuri na Mrisho Ramadhani Kibwigiri.
Kanda namba tano ya Geita, Kagera, Mara na Mwanza waliochukua na kuridisha ni Salum Umande Cham, Vedastus Lufano na Salum Alli Kulunge.
Kanda ya mwisho ya sita inayohusishwa mikoa ya Katavi, Kigoma, Rukwa na Tabora waliochukua na kurudisha ni Blassy M Kiondo, Issa Bukuku na Kanneth Pesambili.