Kijo kocha mpya Zanzibar Sand Heroes

Muktasari:
- Ali Shariff Adolf ambaye alikuwa Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Ufukweni Zanzibar (Zanzibar Sand Heroes) na kuichezea timu ya Malindi, alifariki dunia, Ijumaa Juni 6, 2025.
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF), limemteua Kijo Nadir Nyoni kuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Zanzibar ya Soka la Ufukweni.
Taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Juni 27, 2025 na Ofisa Habari wa ZFF, Mohamed Kabwanga, imesema kocha huyo ana diploma C ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika(CAF) na alishawahi kupata mafunzo ya ukocha wa Mpira wa Ufukweni kutoka CAF.
Pia Kijo aliwahi kuwa msaidizi wa Timu hiyo iliyoshiriki mashindano ya Beach Soccer kwa mara ya kwanza yaliyofanyika Kenya mwaka 2002.
Kocha Kijo amewahi kufundisha klabu mbalimbali kisiwani Zanzibar ikiwemo Kundemba FC, Uhamiaji FC na Polisi FC.
Kijo amechukua nafasi ya Ali Shariff Adolf aliyefariki dunia Ijumaa Juni 6, 2025.