Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanawake Russia wapigwa marufuku kufanya ngono Kombe la Dunia

Moscow, Russia. Mwanasiasa wa Russia, Tamara Pletnyova  amewaonya wanawake nchini humo kutojihusisha mapenzi watu wasio Wazungu kwani watoto ambao watazaliwa wanaweza kunyanyasika na kubaguliwa.  

Alisema wanawake nchini humo wanatakiwa kujizuia kufanya mapenzi na wageni wasio Wazungu kwenye fainali za Kombe la Dunia, ambazo zinatarajia kuanza kutimua vumbi leo Alhamisi kwa mechi ya ufunguzi kadi ya wenyeji Russia na Saudia Arabia.

Aliongeza kuwa iwapo watajihusisha na mapenzi na wageni wasio Wazungu, wanaweza kujikuta wametelekezwa, huku wakiwa na watoto waliozaliwa rangi mchanganyiko.

 “Mara nyingi hata wanawake wa Kirusi ambao huwa kwenye mahusianao ya kimapenzi na watu wasio wazungu huishia pabaya” aliongeza Tamara ambaye ni kiongozi wa kamati ya Bunge nchini urusi inayoshughulikia masuala ya familia wanawake na watoto.

Kiongozi huyo alikuwa akizungumza hayo wakati akijibu swali kutoka kituo kimoja cha redio walipokuwa wakijadili kile kinachojulikana “Watoto wa Olympics” walizaliwa baada ya kumalizima mashindano hayo makubwa ya mwaka 1980.

Mwanasiasa huyo alikuwa anarejelea ubaguzi wa rangi uliojitokeza kipindi hicho baada ya kuzaliwa wototo kati ya wanawake wa Russia na wanaume kutoka Afrika, Latini Amerika na Asia.

Hivyo akasisitiza kwamba ni lazima wanawake wa nchi hiyo wazae watoto wenyewe kwa wenyewe kwani kuchanganya rangi kunaweza kuwaletea matatizo watoto watakaozaliwa

Hata hivyo, Pletnyova alimaliza kwa kutoa kauli tata kwamba, angependa wanawake wa Kirusi kuolewa na mtu yeyote bila kujali rangi wala utaifa, lakini kwa kipindi hiki cha fainali huenda mashabiki wengi wakawa wametua nchini humo na virusi jambo ambalo linaweza kuwaathiri.