Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wakazi Dar wazidi kujiachia na mnada mtandaoni, zawadi kemkem

Jijo Pict

Muktasari:

  • Hii imemkuta mkazi wa Goba, Wilaya ya Ubungo, jijini Dar es Salaam, Adam Adam aliyeibuka mshindi wa pikipiki mpya kutokana na droo ya bahati nasibu inayoandaliwa na kampuni ya Piku Africa, ambayo imeendelea kukua kwa kasi.

FURAHA inazidi kuongezeka kwa wakazi wa Dar es Salaam kutokana na kushiriki mnada mtandaoni na kujishindia zawadi mbalimbali na pesa.

Hii imemkuta mkazi wa Goba, Wilaya ya Ubungo, jijini Dar es Salaam, Adam Adam aliyeibuka mshindi wa pikipiki mpya kutokana na droo ya bahati nasibu inayoandaliwa na kampuni ya Piku Africa, ambayo imeendelea kukua kwa kasi.

Katika droo hiyo, washindi wengine pia wamejinyakulia zawadi nono. Nasra Ally amepata runinga ya inchi 55 pamoja na router, huku Jackson Ngonji akijishindia simu janja aina ya Samsung A16 na spika ya Bluetooth ikiwa ni mara yake ya pili kushinda katika jukwaa hilo.

Baada ya kukabidhiwa zawadi yake, Adam amesema ushindi huo umebadilisha maisha yake kwa kiwango kikubwa, akibainisha mchango wake mdogo umegeuka kuwa bahati isiyo na kifani.

“Nina furaha kubwa kushinda zawadi hii ya pikipiki. Nitaitumia kwa shughuli zangu za kila siku na kama chanzo cha kipato. Hii inadhihirisha bahati huwapendelea wanaojaribu. Niliamua kujaribu  na leo naamini ndoto yangu imekamilika,” amesema.

Kwa upande wake, Ngonji amesisitiza umuhimu wa kuwa na uthabiti katika kushiriki.
“Hii ni mara yangu ya pili kuchaguliwa kuwa mshindi. Inadhihirisha jukwaa hili linaendeshwa kwa uwazi na usawa na ninashukuru kwa zawadi hizi,” amesema kwa furaha.

Afisa Mawasiliano na Mahusiano ya Umma wa kampuni hiyo,Barnabas Mbunda amewapongeza washindi na kuwatia moyo Watanzania wengi zaidi kushiriki na kusisitiza droo hiyo imebuniwa ili kubadilisha michango midogo ya washiriki kuwa zawadi kubwa zisizo za kawaida.

“Lengo letu ni kuwapa watu fursa ya kuota ndoto kubwa na kufanikisha makubwa kupitia juhudi ndogo. Orodha inayoongezeka ya washindi ni ushahidi wa ndoto hiyo,” amesema.

Joram Mtafya, mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), ameipongeza kampuni hiyo kwa kufuata taratibu za michezo ya kubahatisha na kuhakikisha uwazi. Pia aliwapongeza washindi na kuhamasisha Watanzania wengi zaidi kushiriki kwenye michezo ya kubahatisha iliyo halali na yenye usimamizi sahihi.

Kwa ushuhuda wa washindi na uwazi katika uendeshaji, droo ya bahati nasibu ya kampuni hiyo inaendelea kupata umaarufu mkubwa nchini kote, ikiweka matumaini kwa Watanzania wengi kuwa ndoto zao zinaweza kufanikishwa kupitia bahati nasibu hii.