Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dickson Mhilu arudi Kagera Sugar

MHILU Pict
MHILU Pict

Muktasari:

  • Msimu ulioisha, Mhilu ameichezea Dodoma Jiji iliyomaliza nafasi ya tisa kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 35, nyota huyo  baada ya kumaliza mkataba wake akaamua kurejea Kagera inayonolewa na kocha Juma Kaseja.

BAADA ya Kagera Sugar kurejea Ligi Kuu Bara, imeendelea kuimarisha kikosi chake kwa kusajili wachezaji mbalimbali kati ya hao ni Dickson Mhilu aliyesaini mkataba wa miaka miwili hadi 2028.

Msimu ulioisha, Mhilu ameichezea Dodoma Jiji iliyomaliza nafasi ya tisa kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 35, nyota huyo  baada ya kumaliza mkataba wake akaamua kurejea Kagera inayonolewa na kocha Juma Kaseja.

Rafiki wa karibu na mchezaji huyo, amesema Dickson aliona arejee kuongeza nguvu katika timu iliyochangia kukuza kipaji chake na aliipiga chini ofa mpya ya Dodoma. “Alianza kufanya mazungumzo na Kagera mara baada ya kupanda Ligi Kuu, hivyo ikawa rahisi kwake kukubaliana na ofa hiyo na anaona ni timu ya nyumbani,” amesema rafiki yake huyo.

Alipotafutwa kaka yake na Dickson ambaye ni Yusuf Mhilu aliyeipandisha daraja Geita Gold, amesema anachojua mdogo wake amerejea Kagera, ingawa hawezi kuelezea kiundani zaidi.

“Nadhani amesharejea Kagera, lakini sina taarifa zake zaidi kumuhusu kwani msimu ulipomalizika kila mtu alipata nafasi ya kupumzika na kutenga muda wa kujua anaenda wapi,” amesema.

Mhilu anayecheza beki wa kulia, amewahi kucheza Kagera Sugar kabla ya kutimkia Tanzania Prisons na baadaye Dodoma Jiji.