Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vurugu viwanjani mambo ya kishamba

VURUGU Pict

Muktasari:

  • Sio vitendo vya kuviunga mkono na ni vya ovyo sana kwani vinachafua taswira ya nchi yetu kiujumla huku pia likiacha athari nyingine nyingi hasi.

POLE kwa mashabiki wote ambao walikutana na kadhia ya kupigwa, kuchaniwa jezi au kufanyiwa kitendo chochote kisicho cha kiungwana kwenye mechi ya Simba dhidi ya RS Berkane ya Morocco, Jumapili iliyopita kwenye Uwanja wa New Amaan, Zanzibar.

Sio vitendo vya kuviunga mkono na ni vya ovyo sana kwani vinachafua taswira ya nchi yetu kiujumla huku pia likiacha athari nyingine nyingi hasi.

Soka ni mchezo ambao mara zote unahimiza suala la uungwana na upendo hivyo haipaswi kuruhusu matukio kama haya ya kuchania watu jezi, kupiga watu na kadhalika.

Kijiweni hapa tumechukizwa kwa kiasi kikubwa na kilichotokea ambacho kimsingi linaweza kuwa lilichangiwa na kauli zisizo za kiungwana za baadhi viongozi wa Simba kuelekea mechi hiyo. Ni jambo la kipuuzi na linalotakiwa kukemewa kwani linajenga utamaduni ambao kiasili sio wetu Watanzania bali zamani tulikuwa tunausikia tu au kuuona katika nchi nyingine.

Baada ya kijiwe kulaani, tunatakiwa kuhimiza mambo ambayo yanaweza kuwa suluhisho la kupunguza au kumaliza kabisa matatizo haya ya vurugu viwanjani ambayo sasa yanaonekana yanazidi kuchipua tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Kwanza tuanze utamaduni wa kutenganisha majukwaa ya timu tofauti. Kama timu A ikiwa nyumbani inacheza na timu B basi kuwe na majukwaa yatakayowatofautisha mashabiki wa timu hizo mbili na kama shabiki wa timu moja anataka kwenda jukwaa la timu nyingine basi asivae jezi ya timu pinzani au asitoe lugha za kukera au kukejeli wapinzani

Katika mpira wa miguu hisia ni ngumu kuzidhibiti na ndio maana hata mamlaka kubwa za soka zikaweka utaratibu wa kuwepo majukwaa na utaratibu maalum kwa mashabiki wa timu ya nyumbani na ugenini. Walijua sio kazi rahisi kudhibiti mahaba ya watu kwa timu zao.

Jambo la pili ni viongozi kuacha kutoa kauli za uchochezi na pia mashabiki kujitahidi kujizuia na kujilinda kwa kutokaa katika majukwaa ya wapinzani wao.