Vigogo wa wavurugwa Europa Ligi

Muktasari:
Mashindano hayo yapili kwa ukubwa kwa hatua ya klabu barani Ulaya
Milan, Italia. Shaka AC Milan baada ya kulazimishwa suluhu na AEK Athens kwa mara ya pili ndani ya siku 14 katika Europa Ligi jana, huku Everton ikiondolewa mashindano kwa kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Olympique Lyonnais.
Miamba hiyo ya Ufaransa ilitumia vizuri dakika 25 za kipindi cha pili kufunga mabao yake na kuicha Everton ikishikiria mkia wa Kundi E na pointi mmoja na kupoteza nafasi ya kusonga mbele ikiwa na mechi mbili mkononi.
Bertrand Traore alifungia Lyon bao la kuongoza dakika 68, wakati alipomtoka Ashley Williams na kuwahi mpira uliokuwa ukipigwa jwa kipa Jordan Pickford na kufunga goli hilo.
Houssem Aouar alifunga bao la pili akipokea pasi ya Memphis Depay kabla ya Depay kupachika bao la tatu dakika ya 90. Katika siku hiyo mbaya kwa Everton ilishudia beki wake Morgan Schneiderlin akitolewa nje kwa kupata kadi mbili za njano zikiwa zimebaki dakika 10 kabla ya filimbi ya mwisho.
Lyon inaungana na Atalanta kileleni wakiwa na point inane baada ya timu hiyo ya Serie A kuruhusu bao la dakika za mwisho na kulazimishwa sare 1-1 na Apollon ya Cyprus.
Milan imebaki kileleni mwa Kundi D ikiwa na pointi 8, mbili zaidi ya mahasimu wao kutoka Ugiriki, hivyo sasa wanalazimika kushinda mechi zilizobaki ili kumuondolea presha kocha wake Vincenzo Montella.
Dinamo Kiev imekuwa timu ya kwanza kufuzu kwa hatua ya 32 bora baada ya kushinda bao 1-0 dhidi ya Young Boys shukrani kwa goli la Vitaliy Buyalskiy katika mchezo wa Kundi B.
Bao la Carlos Bacca na lile la kujifunga Simon Deli yalitosha kuwapa Villarreal ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Slavia Prague na kuwafanya Wahispania hao kuwa vinara wa Kundi A wakiwa na pointi nane.