VIDEO: Watoto Tanzania watinga nusu fainali Kombe la Dunia wakiibamiza Marekani mabao 5-0
Muktasari:
- Tanzania inakwenda nusu fainali ikiwa haijapoteza hata mchezo mmoja na ikiwa haijafungwa hata goli moja yani clean sheet katika mashindano haya yaliofanyika nchini Urusi mjini Moscow katika Uwanja wa klabu kubwa ya soko nchini Urusi ya Lokomotive Moscow
Timu ya Tanzania iliyopo katika mashindano ya Kombe la Dunia la Watoto wa mazingira magumu yalioandaliwa na Shirika la Street Child United kwa programu ya Street Chil World Cup: Future Depends on You imeibuka na ushindi wa mabao 5-0 baada ya kuibamiza na kuisambaratisha bila ya huruma timu ya Marekani leo asubuhi katika mchezo wa kwanza wa robo fainali.
Tanzania inakwenda nusu fainali ikiwa haijapoteza hata mchezo mmoja na ikiwa haijafungwa hata goli moja yani clean sheet katika mashindano haya yaliofanyika nchini Urusi mjini Moscow katika Uwanja wa klabu kubwa ya soko nchini Urusi ya Lokomotive Moscow.
Vijana hao wa Tanzania wanapambana kila namna ili wachukue tena ubingwa mwaka huu na kutetea taji lake kama ilivyokuwa mwaka 2014 walipokuwa mabingwa nchini Brazil.
Tanzania imeweka heshima na historia kubwa katika kuelekea fainali za Kombe la dunia mwaka huu nchini Urusi.