Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

VIDEO: Hiki ndio chanzo cha kifo cha Mzee Mkapa

Muktasari:

Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa alifariki dunia usiku wa kuamkia Julai 24, 2020 jijini Dar es Salaam na atazikwa Julai 29 kijijini kwao Lupaso wilayani Masasi, Mtwara.

Familia ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa imeweka hadharani chanzo cha kifo chake, ikisema kimesababishwa na shambulio la moyo.

Akizungumza wakati wa misa ya kumuaga Mzee Mkapa katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam msemaji wa familia, William Erio amesema awali alikuwa hajisikii vizuri na alipopelekwa hospitali baada ya vipimo alikutwa na malaria.

“Alianza matibabu na kulazwa siku ya Jumatano Julai 22, 2020 na Alhamisi mchana aliendelea vizuri na nilikuwa naye akanipa maagizo ya kwenda kumpa Baba Askofu, Nzigilwa kuhusu kushindwa kuhudhuria shughuli ya kumuaga jana,” amesema Erio, ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii, NSSF.

Amesema kabla ya umauti, Mzee Mkapa alikuwa akifuatilia mchakato wa kupata wagombea kwa upande wa viti maalum mubashara kwenye luninga kisha akaangalia taarifa ya habari na kuagana naye.

“Baada ya hapo taarifa inasema baada ya kuangalia taarifa ya habari aliinuka akataka kutoka, ila alikaa akainamisha kichwa hadi wakaja kumpima ikathibitika alishafariki dunia”.