Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vibali vyamweka nje beki Ceasiaa

VIBALI Pict

Muktasari:

  • Adongo alijiunga na Ceasiaa dirisha dogo baada ya kupewa mkono wa kwaheri na Alliance Girls alikodumu kwa takriban misimu mitano tangu aliposajiliwa msimu 2019/20.

BEKI wa kati wa Ceasiaa Queens, Anita Adongo amesema yuko nje ya uwanja kwa takribani miezi miwili kwa changamoto ya vibali ambayo huenda akaanza kucheza msimu ujao.

Adongo alijiunga na Ceasiaa dirisha dogo baada ya kupewa mkono wa kwaheri na Alliance Girls alikodumu kwa takriban misimu mitano tangu aliposajiliwa msimu 2019/20.

Akizungumza na Mwanaspoti, Adongo alisema kwa sasa anaendelea na mazoezi na timu hadi atakapokamilishiwa vibali vya kucheza Ligi Kuu.

"Siumwi, lakini kuna changamoto za vibali ndiyo inakwamisha hadi leo sijacheza mechi yeyote, nafanya mazoezi na timu, yakikamilika nafikiri nitaonekana uwanjani kwa sasa nipo tu kambini."