Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Unamtaka Messi? Sahau kabisa

Muktasari:

Jambo hilo linatarajiwa kufanyika wiki chache zijazo ambapo, kwa sasa Messi na kipenzi chake mrembo Antonella Roccuzzo wapo mapumzikoni baada ya kazi nzito ya msimu uliopita na michuano ya Copa America 2016.


BARCELONA imeshtukia chokochoko za Chelsea juu ya supastaa wao Lionel Messi na hivyo, wanaamua kumpa mwanasoka huyo mkataba mpya wa miaka mitano ambao utamfanya abaki kwenye kikosi chake hadi atakapofika umri wa miaka 33.

Messi anahusishwa na mpango wa kutimkia Chelsea baada ya baba yake kukutana kwa siri na bilionea wa klabu hiyo ya Ligi Kuu England, Roman Abramovich katika meli yake ya kifahari.

Kwa mujibu wa gezeti la michezo la Hispania, Mundo Deportivo, miamba hiyo ya Calatan inataka kumpiga kitanzi Messi na kumfanya abaki kwenye timu yao hadi mwaka 2021.

Jambo hilo linatarajiwa kufanyika wiki chache zijazo ambapo, kwa sasa Messi na kipenzi chake mrembo Antonella Roccuzzo wapo mapumzikoni baada ya kazi nzito ya msimu uliopita na michuano ya Copa America 2016.

Mkataba wa sasa wa Messi unafika tamati 2018 na kwamba, kuna kipengele kilichoandikwa Euro 250 milioni kwa timu itakayohitaji saini ya staa huyo wa kimataifa wa Argentina.

Bado haijafahamika Messi atalipwa kiasi gani katika mkataba wake huo mpya wakati kwa sasa akiwa anapokea Pauni 336,000 kwa wiki. Messi ametwaa tuzo tano za Ballon d’Or.

Barca pia ina mipango ya kumbakiza Javier Mascherano kwa kumpa mkataba mpya utakaomfanya aendelee kubaki kwenye kikosi hicho kwa muda mrefu baada ya kufurahishwa na soka lake. Hivi karibuni Barca ilimwongeza mkataba mpya staa wao wa Kibrazili, Neymar ambaye alikuwa akihusishwa na mpango wa kujiunga na Manchester United na mabingwa wa Ufaransa, PSG.