Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ibenge ameanza na hili Azam FC

IBENGE Pict

Muktasari:

  • Ibenge, ambaye ni kocha mwenye uzoefu wa soka la Afrika na ametwaa mataji mbalimbali kimataifa akitoka kuipa ubingwa wa ligi Al Hilal ya Sudan, alisisitiza nidhamu ndiyo msingi wa mafanikio ya timu yoyote na malengo yake ni kuipambania timu hiyo iwe miongoni mwa timu bora Afrika.

BAADA ya kukabidhiwa mikoba ya kuinoa Azam FC, Florent Ibenge ameanza rasmi kueleza mikakati na misimamo yake ya kazi kikosini na ameweka wazi nidhamu ndiyo kipaumbele cha kwanza kwa mchezaji kupata namba kikosi cha kwanza.

Ibenge, ambaye ni kocha mwenye uzoefu wa soka la Afrika na ametwaa mataji mbalimbali kimataifa akitoka kuipa ubingwa wa ligi Al Hilal ya Sudan, alisisitiza nidhamu ndiyo msingi wa mafanikio ya timu yoyote na malengo yake ni kuipambania timu hiyo iwe miongoni mwa timu bora Afrika.

Akizungumza na Mwanaspoti, Ibenge alisema uhakika wa kuwa na kikosi bora kutokana na mafanikio ya timu hiyo msimu huu kumaliza nafasi ya tatu anao lakini bado hana nyota wa kikosi cha kwanza hivyo ili kupata kikosi bora cha kuipa mataji timu hiyo nidhamu ndiyo kipaumbele cha kwanza.

“Nidhamu ndiyo msingi imara kwenye maisha ya kila mwanadamu bila kujali anafanya jukumu gani kwangu kwenye mpira mafanikio niliyoyapata kwenye mataifa yote niliyoyafundisha msingi wangu bora ni huo sambamba na kufanya kazi kwa ushierikiano,” alisema na kuongeza;

“Nimekubali kufanya kazi na Azam FC ambayo imeanza kunishawishi muda mrefu na nipo tayari kuipa mafanikio na kuifanya timu bora Afrika ukizingatia ni timu ambayo imejijenga kwenye kila kitu ina uwanja na fedha ya kujiendesha naahidi kuifanya kuwa miongoni mwa timu bora nikihitaji ushirikiano wa kutosha kutoka kwa viongozi, wachezaji na mashabiki;

“Kama unataka mafanikio, tunahitaji wachezaji wanaojitambua na wanaothamini kuvaa jezi yenye nembo ya klabu, muda wa kucheza soka ni mfupi nidhamu bora kwenye uwanja na nje ya uwanja ndiyo vitakavyosaidia mafanikio ya klabu naamini nitafanya kazi vizuri na wachezaji ili kuweza kufikia mafanikio,” alisema kocha huyo ambaye amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuinoa Azam FC.

Ibenge amesaini mkataba huo na anajiunga na timu hiyo kuchukua mikoba ya Rachid Toussi ambaye amemtaja kuwa ni rafiki yake na kumpongeza kwa mafanikio aliyoyaacha akiipa timu hiyo nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao Kombe la Shirikisho Afrika.