Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Unaijua tofauti ya Kiiza, Tambwe na Kipre?

Hamis Kiiza si mfungaji asilia kama Tambwe. Wala si mviziaji mzuri. Lakini ni mpiganaji asilia kuliko Tambwe.

Muktasari:

  • Kwa ulaya, Tambwe ni aina ya wafungaji kama Ruud van Nisterlooy, Fillipo Inzaghi na Mario Jardel. Kwa aina ya wachezaji wa sasa unaweza kumlinganisha na Javier Hernandez ‘Chicharito’

KILA siku unasogea Uwanja wa Taifa, unalipa tiketi, unaingia uwanjani na unashuhudia mabao. Wafungaji watatu wa klabu za Azam, Simba na Yanga, Kipre Tchetche, Amissi Tambwe na Hamis Kiiza ‘Diego’ wanafunga kila mara unajua tofauti yao?

Tambwe, mwizi mkamilifu

Katika wote hawa, Tambwe ndiye mwizi mkamilifu. Alizaliwa kwa ajili ya kufunga. Nje ya eneo la 18, hajui sana soka. Ndani ya eneo la 18 anajua lango lilipo na anajua nyavu zilipo. Amefunga mabao mengi ya penalti, lakini angeweza kufunga mabao mengi ya muvu za kawaida (open play) kama angeikuta Simba yenye uwezo wa kupika mabao chini ya Emmanuel Okwi na Mwinyi Kazimoto.

Aina yake ya mabao ni kama ya Jerrson Tegete alipokuwa katika kiwango, au kama ni miaka michache nyuma basi unaweza kusema Emmanuel Gabriel. Ukirudi nyuma kidogo unaweza kumfananisha na Mohamed Hussein.

Kwa ulaya, Tambwe ni aina ya wafungaji kama Ruud van Nisterlooy, Fillipo Inzaghi na Mario Jardel. Kwa aina ya wachezaji wa sasa unaweza kumlinganisha na Javier Hernandez ‘Chicharito’

Tatizo anacheza katika kikosi cha Simba kisichokuwa na huduma sana. mabeki wa pembeni wa Simba, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ na Said Chollo au Haruna Shamte hawapo katika ubora wa Ramadhan Wasso au Said Sued. Nyuma yake wakicheza Abdulhalim Humoud au Jonas Mkude pasi nyingi zinakwenda pembeni.

Kuibuka kwake kuwa mfungaji bora mwishoni mwa msimu kutategemea zaidi jinsi Simba watakavyochanga karata zao katika kusajili viungo washambuliaji makini. Lakini wakati mwingine suluhisho halitoki nje ya timu tu, je kocha yoyote atakayeiongoza Simba katika mzunguko wa pili, atajua namna ya kumtengenezea nafasi?

Kiiza mpiganaji wa vitani

Hamis Kiiza si mfungaji asilia kama Tambwe. Wala si mviziaji mzuri. Lakini ni mpiganaji asilia kuliko Tambwe. Inashangaza Yanga walikuwa wanataka kuachana naye dirisha lililopita. Mnaweza kuwauliza, hivi huwa wanavuta nini pale Jangwani?

Wakati Tambwe ni bora zaidi katika eneo la ndani, Kiiza ana msaada ndani na nje ya lango. Tatizo la kiasili ni moja. Washambuliaji wengi wenye uwezo wa kupigana nje ya lango huwa hawana shabaha nzuri. Kiiza ni mmojawapo. Katika dunia ya kileo, washambuliaji wawili niliwaona wakiwa wamekamilika katika upiganaji na shabaha, Ronaldo de Lima na Didier Drogba.

Uzuri wa Kiiza ni kwamba katika timu yake kuna huduma timilifu. Muda wowote Athuman Idd ‘Chuji’ anaweza kupiga pasi ndefu kwa Simon Msuva au Mrisho Ngassa. Winga yoyote kati ya hawa akipiga krosi ya karibu, Kiiza anacheka.

Didier Kavumbagu pia ni mchezeshaji mzuri kutokana na umbo lake kubwa na ugomvi wake mkubwa dhidi ya mabeki wagumu. Anajikuta katika nafasi nzuri ya kutengeneza nafasi kwa wenzake waliosahauliwa. Jiulize kama Tambwe angecheza na Ngassa, Kavumbagu au Msuva!

Yanga pia wanaweza kutengeneza nafasi kupitia kwa walinzi wao wa nyuma, Twitte na David Luhende. Wote ni wazuri katika kupanda mbele. Timu yao imekaa pamoja muda mrefu na wanajiamini zaidi.

Lakini pia Yanga wanaweza kutengeneza mabao hata kwa mipira ya kurushwa ya Mbuyu Twitte. Ni aina hii hii ya mipira ya kurushwa ndio ambayo Kiiza amewaliza Juma Kaseja na Abel Dhaira katika mechi mbili zilizopita za watani wa jadi.

Kipre Tchetche amekamilika zaidi

Weka wote hao wawili pembeni, Kipre Tchetche wa Azam amekamilika zaidi. Asikuambie mtu. Kipre ana uwezo wa kuwa muunganiko wa Kiiza na Tambwe. Ana uwezo mkubwa wa kupigana nje ya eneo la hatari, na hapo hapo ana uwezo wa kufunga.

Bao alilomfunga Dhaira katika pambano dhidi ya Simba lilithibitisha ubora wake katika kutulia na kufunga kama Tambwe anavyofanya. Lakini hapo hapo, jinsi alivyokimbia na mpira kutoka mbali inathibitisha kwamba anaweza kupigana kama Kiiza anavyofanya.

Tatizo la Kipre ni kwamba kocha wake anakosea jinsi ya kumtumia. Katika mfumo wa 4-3-3, Kipre anachezeshwa pembeni, John Bocco anapangwa kati, na katika upande wa kushoto anapangwa chipukizi Joseph Kimwaga.

Kipre anajikuta yuko mbali na lango. Mabao yake yanatokana zaidi na juhudi zake binafsi kuliko kuchezeshwa. Kama vile haitoshi, Kipre hapati huduma nyingi kama wanazopata washambuliaji wa Yanga ambao siku zote wanafunga mabao rahisi.

Mfumo wa Stewart Hall mara nyingi unatumia viungo watatu uwanjani. Walinzi wawili wako nyuma sana na pasi zao hazina madhara. Hawa ni Salum Abubakar na pacha wa Kipre, Michael Balou.

Chukua mfano wa Sure Boy. Huyu si kiungo mshambuliaji na wala si kiungo wa ulinzi. Kazi yake kubwa ni kupiga pasi nyingi za kutawala mchezo. Lakini hana madhara sana kwa sababu anapiga pasi za pembeni zaidi (Square pass) na hapigi pasi za mwisho.

Kiungo mwingine, HumpHrey Mieno anacheza taratibu sana na wala hana uhodari mkubwa katika kupika mabao. Shukrani zianze kwenda kwa kinda Kimwaga ambaye kasi yake inaweza kumsaidia Kipre kama ilivyojitokeza katika mechi Ruvu Shooting.