Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Uchukuaji fomu TFF wafungwa kwa malalamiko

Oscar Oscar akizungumza na wandishi wa habari baada ya kurudisha fomu ya kugombea nafasi ya urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).Picha na Michael Matemanga

Muktasari:

Zoezi la uchukuaji na urejeshaji fomu kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limefungwa rasmi huku wagombea wengi wakilalamikia kipengere cha udhamini kuwa kikwazo.

Zoezi la uchukuaji na urejeshaji fomu kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limefungwa rasmi huku wagombea wengi wakilalamikia kipengere cha udhamini kuwa kikwazo.

Wagombea urais, Oscar Oscar na Ally Salehe sanjari na wale wa ujumbe, Saady Khimji na Joseph Mnangwa kwa nyakati tofauti wamesema kipengere hicho hakikuwa fear kwa wengine.

Moja ya kanuni za uchaguzi huo inataka mgombea urais kuwa na wadhamini kuanzia watano huku kwenye ujumbe inamtaka mgombea kuwa na mdhamini mmoja.

Oscar kwa upande wake amedai amerejesha fomu bila kuwa na mdhamini huku Ally amesema kwake kupata udhamini ilikuwa ni tatizo japo amefanikisha kuwapata watano.

Khimji amesema klabu yake ya Yanga imemdhamini japo mwanzo alitarajia kupata udhamini wa mkoa wa Dar es Salaam akakuta tayari mgombea Lameck Nyambaya amemuwahi.

Wakati Joseph akidai kuna uwezekano baadhi ya wagombea wakaenguliwa kwa kukosa udhamini wakati ni watu wa mpira.

Mchakato wa uchukuaji na urejeshaji fomu umefungwa rasmi jioni hii kupisha michakato mingine kuelekea kwenye uchaguzi huo wa Agosti 7 mkoani Tanga.