Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TWFA Mwanza yapata mabosi wapya

Muktasari:

  • Tigalyoma amerejea kwenye nafasi hiyo tena baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi huo uliofanyikwa leo Jumamosi kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kuanzia saa 4:00 hadi 4:50 asubuhi kwa kupata kura saba kati ya 10 zilizopigwa, huku Makilagi akiambulia kura tatu tu.

SOPHIA Tigalyoma amechaguliwa kuwa Mwenyekiti Mpya wa Chama cha Soka la Wanawake (TWFA) Mkoa wa Mwanza akimbwaga aliyekuwa mtetezi wa kiti hicho Sophia Makilagi.

Tigalyoma amerejea kwenye nafasi hiyo tena baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi huo uliofanyikwa leo Jumamosi kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kuanzia saa 4:00 hadi 4:50 asubuhi kwa kupata kura saba kati ya 10 zilizopigwa, huku Makilagi akiambulia kura tatu tu.

Makilagi alikiongoza chama hicho kwa miaka minne kuanzia 2020 akimng'oa Tigalyoma ambaye leo amerejesha nafasi yake na atakiongoza chama hicho hadi 2028.

Katika nafasi ya Wajumbe wa kamati ya Utendaji ya chama hicho, Hawa Bajanguo na Flora Gaguti walishinda kwa kupata kura saba kila mmoja, wakiwashinda Elizabeth Nyingi na Glory Mbise waliombulia kura tatu kila mmoja.

Revina Muzawena ametetea nafasi ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa kwa kupigiwa kura nane akimbwaga Johari Ngassa aliyeambulia kura mbili.

Akizungumza baada ya ushindi huo, Mwenyekiti mpya, Sophia Tigalyoma amesema anakwenda kuchapa kazi, kuwaunganisha wanachama na wadau, kufufua soka la wanawake mkoani humo na kumaliza majungu.

"Mimi na jopo langu tunaingia kuchapa kazi, mnanifahamu nikiingia kazini ni kuchapa kazi nawaahidi kufanya kazi tu. Mimi ni mtu wa kujishusha ni kiongozi napokea ushauri wa kila mmoja. Majungu ni mabaya nina furaha nakwenda kuchapa kazi na kazi mtaiona," amesema bosi huyo mpya wa TWFA Mwanza.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa uchaguzi huo, Alhaji Majogoro, amewataka viongozi waliochaguliwa kufanya kazi kwa bidii, kuwaunganisha wadau wa soka na kuongeza timu za wanawake.

"Tunasuasua katika Ligi Kuu ya Wanawake (WPL), waisaidie Alliance Girls isishuke, pia wazalishe timu nyingine kwa sababu Mwanza ni mkoa mkubwa na kwa sasa tunazo timu 10 tu zilizosajiliwa, kwa hiyo waisaidie Mwanza Queens nayo ipande Ligi Kuu," amesema Majogoro.