Toto, Pamba waiteka Mwanza

Muktasari:
- Pamoja na ukongwe wa Toto Africans, lakini Pamba ndiyo timu yenye mafanikio zaidi katika historia ya soka ya Mwanza
Kitanuka nakwambia ni Mwanza Derby katika Ligi Daraja la Kwanza wakati Pamba FC itakapowaribisha ndugu zao wa Toto Africans.
Pamba itaingia katika mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kipigo cha mabao 4-1 walichokipata kutoka kwa Toto katika mchezo wa Kombe la FA msimu uliopita.
Toto Africans ina pointi nne huku Pamba ikiwa na pointi mbili hivyo mchezo huo utakuwa mgumu kutokana na kila timu kutaka ushindi ili kujiweka vyema kwenye msimamo wa Ligi hiyo kwenye Kundi C.
Kocha wa Pamba, Mathias Wandiba alisema kikosi chake kipo fiti kuwavaa Toto Africans na kuondoka na ushindi katika mchezo huo.
Alisema katika mtanange huo wachezaji wake wawili hawatakuwepo kwenye mchezo huo kutokana na kuwa majeruhi.
“Mshambuliaji Emmanuel Manyanda atakuwepo kikosini kutokana na kuwa na jeraha kwenye sehemu ya mbavu huku Winga Amos Mnyapi akisumbuliwa na enka”alisema Wandiba.
Kocha wa Toto Africans, Almas Moshi alisema kikosi chake kipo tayari kwa mapambano katika mtanange huo.
“Tuko fiti kupambana katika mchezo huo vijana wako vizuri,” alisema kwa kifupi kocha Moshi.