Timu ya Nahreel yazinduka WBDL

Muktasari:
- Dream iliyoanzishwa na Emmanuel Mkono ajulikanaye kwa jina la kisanii kama Nahreel, katika mchezo huo iliishinda Kigamboni Queens kwa pointi 78-49 kwenye Uwanja wa DonBosco uliopo Upanga, Dar es Salaam.
KAMA utani timu ya mpira wa kikapu ya Real Dream iliyoanza kwa kukatisha tamaa mashabiki katika Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (WBDL), imeshangaza wengi ni baada ya kuonyesha kiwango kikubwa katika mchezo dhidi ya Kigamboni Queens.
Dream iliyoanzishwa na Emmanuel Mkono ajulikanaye kwa jina la kisanii kama Nahreel, katika mchezo huo iliishinda Kigamboni Queens kwa pointi 78-49 kwenye Uwanja wa DonBosco uliopo Upanga, Dar es Salaam.
Kiujumla, ilianza vibaya mashindano hayo kwa kufungwa kwa pointi 47-40 na Twalipo Queens kisha ilifungwa na Ukonga Queens kwa pointi 72-61 na baadaye ikafungwa na Jeshi Stars kwa pointi 88-55.
Wakati huo huo, timu ya Tausi Royals inaendelea kuongoza katika Ligi ya WBDL, kwa pointi 10 ikifuatiwa na Vijana Queens iliyopata pointi 9.
Timu zinazofuatia ni DB Lioness iliyopata pointi 9, Twalipo Queens (9), Jeshi Stars (8), DB Troncatti (8), Real Dream (8), Kigamboni Queens (8) na Polisi Stars (7).
Nyingine ni Pazi Queens (7), JKT Stars (6), Ukonga Queens (6), City Queens (6), Mgulani Stars (5), Kurasini Kurasini Divas (5) na UDSM Queens (5).
MSIMAMO (WANAWAKE)
TIMU PLD W L PTS
Tausi Royals 5 5 0 10
Vijana Queens 5 4 1 9
DB Lioness 5 4 1 9
Twalipo Queens 5 4 1 9
Jeshi Stars 4 4 0 8
DB Troncatti 4 4 0 8
Reel Dream 6 2 4 8