The Snipers Pool Club yatwaa ubingwa Pool Table
Mashindano ya robo mwaka mchezo wa Pool Table upande wa Black Ball yamekamilika jijini Dodoma na kuishuhudia klabu ya The Snipers ikiibuka na ushindi kwa kuifunga Moro Pool Club kwa fremu 13-10.
Mchezo huo wa fainali ulionekana kuwa wa kuvutia na wenye ushindani mkali kutokana na ubora wa timu zote mbili.
Mara baada ya kutwaa ubingwa huo, The Snipers Pool Club, wamejinyakulia Kikombe, medali, pamoja na fedha taslimu Sh1 milioni na sh500,00, huku washindi wa pili Moro Combine wakijinyakulia medali, pamoja na fedha taslimu sh1 milioni.
Mlezi wa TAPA Mrisho Mpoto maarufu Mjomba ndie aliyefunga mashindano hayo na kwa kuwakabidhi washindi zawadi katika mashindano hayo yaliyofanyika kwa muda wa siku tatu.
“Nimefurahishwa na viwango vizuri vilivyooneshwa na wachezaji zaidi ya 160 walioshiriki katika wachezaji binafsi pamoja na timu kumi na sita kutoka mikoa sita ya Tanzania Bara pamoja na Visiwani Zanzibar, yamekuwa ni mashindano mazuri kwa sababu wote mmekuja kushindana” alisema Mjomba.