Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TFF kuwanyoosha mashabiki wakorofi

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limekemea vikali vitendo vinavyoendelea vya baadhi ya washabiki kupiga washabiki wenzao na viongozi wa timu pinzani.

Taarifa iliyotolewa na Shirikisho hilo imekemea vikali wale wote wanaofanya vitendo hivyo na imeanza kukusanya ushahidi wa matukio yote ya aina hiyo kupitia kamera za kurekodi matukio (CCTV) zilizoko uwanjani.

Aidha TFF iliwataka watu wote wanaohusika na vurugu kwenye Mpira wa Miguu (washabiki pamoja na viongozi) watachukuliwa hatua kali za kinidhamu.

Ilieleza kuwa wale wote wanaotoa shutuma kwa viongozi na maneno ya kuhamasisha vurugu katika Mpira wa Miguu nao watachukuliwa hatua hizo kwa mujibu wa kanuni zilizopo.

Kanuni kuu ya Mpira wa Miguu ni mchezo wa kiungwana (fair play) ndani na nje ya uwanja, hivyo wadau wote wa Mpira wa Miguu wajiepushe na vitendo vya vurugu ili kulinda heshima ya mchezo huo unaoongoza kwa kuwa na washabiki wengi Duniani.