Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanafunzi walioduwaza wakongwe kikapu taifa

TAIFA Pict

Muktasari:

  • Hicho ndicho ilichofanya timu ya kikapu ya Mkoa wa Dar es Salaam (Dream Team) wanaume na ile ya wanawake ya Mkoa wa Arusha katika mashindano ya Kombe la Taifa yaliyomalizika mjini Dodoma.

KAMA una malengo ya kufanya vizuri katika mashindano cha kwanza unatakiwa ufanye maandalizi ya kutosha na uwe na  wachezaji wenye uwezo mkubwa.

Hicho ndicho ilichofanya timu ya kikapu ya Mkoa wa Dar es Salaam (Dream Team) wanaume na ile ya wanawake ya Mkoa wa Arusha katika mashindano ya Kombe la Taifa yaliyomalizika mjini Dodoma.

Katika mashindano hayo timu ya mpira wa kikapu ya wanaume ya Dar es Salaam na Arusha zilitwaa ubingwa katika michuano hiyo ambayo ilikutanisha mikoa ya Bara na Zanzibar kwenye Uwanja wa Chinangali - Dar es Salaam ikitawazwa bingwa baada ya kuifunga Mara kwa pointi 68-52, huku Arusha ikiifumua Dar es Salaam wanawake kwa pointi 56-50.

Katika mchezo wa nusu fainali Dar es Salaam iliifunga Mtwara kwa pointi 73-53 ilhali Mara ikaifunga Dodoma 78-74.

Kwa upande wa wanawake Dar es Salaam iliifunga Dodoma kwa pointi 172-156, huku Arusha ikiifunga Mbeya 59-36.

Kabla ya mashindano hayo Dar es Salaam (Dream team), ilitabiriwa na wengi kwamba ingebeba ubingwa kutokana na uwezo mkubwa wa wachezaji iliokuwa nao na ubora ligi yake (BDL), huku Arusha iliyowakilishwa na wanafunzi wa Sekondari ya Orkeeswa ambayo haichezi ligi yoyote ikibeba ndoo upande wa wanawake na kuziduwaza timu mbalimbali zilizokuwa na nyota kibao wanaoshiriki mashindano ya ligi za mikoa.

Mbali ya kutocheza ligi, wachezaji wa shule hiyo ndio wanaounda timu ya taifa ya wasichana ya umri wa chini ya miaka 18 na katika mashindano hayo viwango walivyoonyesha vinaonnyesha ni kwa namna gani mabinti hao wanapikwa na kupikika katika michezo, hususan kikapu.

Mmoja wa makocha wa shule hiyo, Ben Ngogo ameliambia Mwanaspoti kwamba, wachezaji waliowakilisha mkoa wa Arusha wote wanatoka katika shule hiyo na wamekuwa wakipikwa kwa namna ya pekee kimichezo.

Baada ya fainali hiyo kumalizika Dares Salaam Arusha walikabidhiwa Sh7 milioni na kombe, huku mshindi wa pili upande wanaume - Mara pamoja Dar es Salaam wanawake wakikabidhiwa Sh4. milioni na kombe.

Mfungaji bora wa wanawake alichaguliwa kuwa Jesca Ngisaise wa Dar es Salaam ilhali wanaume ni Jonas Mushi wa Mara walioondoka na Sh200,000 kila mmoja, huku Omary Ndula wa Dar es Salaam alizawadiwa Sh250,000 baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mashindano hayo (MVP). Zawadi hizo pia alipewa mchezaji Nelious Mbungeni wa Arusha aliyechaguliwa  kuwa mchezaji bora wa mashindano hayo upande wanawake (MVP).

Zawadi zingine zilizotolewa ni Sh200,000 zilizokwenda kwa mchezaji chipukizi Rose Katamboy wa Arusha na mzuiaji bora Jimmy Brown wa wa Dar es Salaam. Na upande wa makocha wanaume alichaguliwa Miyasi Nyamoko wa Mara, huku kwa wanawake alikuwa ni Catherbert Maganga kutoka Arusha.