Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TETESI ZA MASTAA ULAYA: Chelsea, Man United zamsubiri Ramsey

Muktasari:

  • Katika dirisha kubwa la majira ya joto Arsenal walikataa dau la pauni 50 milioni kwa Ramsey wakiamini kwamba wangemalizana naye lakini sasa mazungumzo baina yao yamevunjika baada ya Arsenal kugoma kutoa dau kubwa la mshahara katika madai ya sasa. Pia wachezaji katika timu mbalimbali barani Ulaya tayari wameanza kusikika kwenye anga za usajili wa dirisha dogo linalokaribia la Januari.

KIUNGO wa Arsenal, Aaron Ramsey, 27,  sasa anajiandaa kuondoka Arsenal mwishoni mwa msimu huu baada ya kuvunjika kwa mazungumzo kati yake na klabu hiyo na klabu za Chelsea na Manchester United zimekuwa zikimnyatia.

Kwa muda mrefu sasa wawakilishi wa staa huyo wa kimataifa wa Wales wamekuwa katika mazungumzo na Arsenal lakini sasa imebainika kwamba hakuna kinachoendelea na mchezaji huyo ataondoka bure mwishoni mwa msimu huu.

 

Paul Pogba

KIUNGO mahiri wa Manchester United, Paul Pogba amepania kuondoka Old Trafford bila ya kujali kama kocha wake, Jose Mourinho ataendelea kuwa kocha mkuu au ataondolewa klabuni hapo.

Pogba yupo katika bifu kali na Mourinho huku akiwa amemwambia kocha huyo na uongozi wa United kwamba anataka kuondoka klabuni hapo na sasa imebainika kwamba amepania kuondoka hata kama Mourinho ataondoka Trafford.

 

Sadio Mane

MASTAA wawili wa Liverpool, Sadio Mane na James Milner bado hawajakaribia kusaini mikataba mipya Anfield ingawa klabu hiyo inataka kuwapatia mikataba mipya ya kuendelea kukipiga klabuni hapo.

Mkataba wa Milner unamalizika mwaka 2020 huku wa Mane ukitarajiwa kumalizika mwaka 2021 lakini mpaka sasa hakuna mazungumzo ya mikataba mipya kwa mastaa hao na Liverpool haina haraka.

 

 Tanguy Ndombele

MANCHESTER United imeendelea kutuma maskauti wake kwa kiungo mahiri wa Lyon ya Ufaransa, ​Tanguy Ndombele anayekipiga katika kikosi cha Ufaransa chini ya umri wa miaka 21 huku pia akitakiwa na Tottenham.

Ndombele, 21, amesaini mkataba wa miaka mitano na Lyon mapema mwezi huu lakini jambo hilo halijawashtua City na wameendelea kumchunguza staa huyo ambaye aliwasumbua katika pambano la Ligi ya mabingwa hivi karibuni.

 

Ismaila Sarr

CHELSEA na Tottenham zimejiunga katika mbio za kumsaka winga mahiri wa Rennes ya Ufaransa, Ismaila Sarr, 20 ambaye imebainika kuwa amekuwa akifukuziwa kwa karibu na timu nyingine ya London, Arsenal.

Staa huyo wa kimataifa wa Senegal ambaye aling’ara katika michuano ya kombe la dunia nchini Russia mpaka sasa ameifungia Rennes mabao matatu katika michuano mbalimbali nchini Ufaransa na amekuwa akifananishwa na Ousmane Dembele wa Barcelona.

 

Eder Militao

EVERTON wanavutika na mpango wa kumnasa mlinzi wa kulia wa Porto na timu ya taifa ya Brazil, Eder Militao, ambaye vile vile ana uwezo wa kucheza kama mlinzi wa kati.

Maskauti wa Everton walimchunguza mlinzi huyo katika pambano la Porto dhidi ya Vitoria Setubal Jumamosi, lakini pia walimtazama katika pambano la Ligi ya mabingwa wa Ulaya dhidi ya Schalke katikati ya wiki iliyopita.

 

Jerome Boateng

IMEBAINIKA kwamba bodi wa Manchester United ilimzuia kocha wao, Jose Mourinho kumchukua mlinzi wa Bayern Munich, Jerome Boateng katika dirisha kubwa lililopita la uhamisho.

Baadaye nusura mlinzi huyo wa kimataifa wa Ujerumani mwenye asili ya Ghana ahamie PSG lakini hata hivyo dili hilo halikutokea licha ya Bayern kumruhusu kuondoka klabuni hapo huku wakipanga dau la pauni 40 milioni kumuuza.

 

Ryan Astley

ARSENAL wanamnyemelea kinda mahiri wa Everton, Ryan Astley, 16 baada ya Everton kushindwa kumpa mkataba wa soka la kulipwa mpaka sasa ingawa sasa watapambana zaidi kwa ajili ya kuikwamisha Arsenal.

Astley ambaye ni mlinzi wa kati anaingia miaka 17 mwezi ujao na anatajwa kuwa mmoja kati ya makinda bora klabuni hapo katika kikosi cha chini ya umri wa miaka 23 ambacho kinafundishwa na staa wa zamani wa timu hiyo, David Unsworth.

 

Ivan Rakitic

PSG iliorodhesha orodha ya viungo ambao iliwataka katika dirisha kubwa lililopita wakiwemo, Ivan Rakitic wa Barcelona, N'Golo Kante  wa Chelsea na staa wa Lazio na timu ya taifa ya Serbia, Sergej Milinkovic-Savic.

 Hata hivyo wachezaji hao walikuwa ghali na iliangalia pia uwezekano wa kuwanasa wengine kama Marouane Fellaini, Axel Witsel, Fred na Renato Sanches lakini pia dili zao zikashindikana.