Tanzania, Sudani Kusini hakuna mbabe
DAKIKA 45 za kipindi cha kwanza zimemalizika kwa timu ya Tanzania kutoka sare ya 0-0 dhidi ya Sudani Kusini katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la CECAFA kwa vijana chini ya miaka 23 mchezo unaofanyika katika uwanja wa Bahir Dar nchini Ethiopia.
Katika mchezo huo Tanzania imeonekana kumiliki mpira katika dakika 15 za mwanzo za mchezo kwa kukosa umakini katika safu ya umaliziaji kabla ua Sudani kujibu mapigo kwa kuliandama lango la Stars huku golikipa Wilbol Maseke akiokoa nafasi kadhaa ambazo timu hiyo imepata.
Mchezo umeonekana kuwa na ushindani mkubwa huku kila timu ikicheza kwa tahadhari huku Tanzania ikionekana kufika langoni mwa Sudani Kusini mara kwa mara na kuonekana wazi kuhitaji kucheza fainali ya michuano hiyo endapo wataibuka na ushindi.
Sudani Kusini ambayo imeshinda michezo yote miwili iliyopita katika hatua ya makundi imeonekana kupata wakati mgumu chini ya vijana wa kocha Kim Poulsen kutokana na umakini na umiliki mpira kwa asilimia kubwa.