Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanzania kuandaa Afcon 2017

Kabumbu

Muktasari:

Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Celestin alisema jana kuwa wamejiridhisha kuwa wanaweza kuandaa fainali hizo ; “Tuna uwanja wa Taifa, lakini kuna viwanja kama Arusha, Mwanza na Zanzibar, viwanja hivi vikiboreshwa na hoteli tulizonazo, tunaweza kuandaa fainali hizi, tumeandaa maombi yetu na tutayapeleka Serikalini kwa ajili ya kupata baraka.”

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetangaza nia ya kuandaa fainali za Mataifa ya Afrika za 2017 baada ya kujitoa kwa Libya kutokana na sababu za kiusalama.

Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Celestin alisema jana kuwa wamejiridhisha kuwa wanaweza kuandaa fainali hizo ; “Tuna uwanja wa Taifa, lakini kuna viwanja kama Arusha, Mwanza na Zanzibar, viwanja hivi vikiboreshwa na hoteli tulizonazo, tunaweza kuandaa fainali hizi, tumeandaa maombi yetu na tutayapeleka Serikalini kwa ajili ya kupata baraka.”

Katika hatua nyingine, TFF imemteua aliyekuwa msemaji wake, Boniface Wambura kuwa Mkurugenzi wa mashindano. Wambura anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Saad Kawemba ambaye aliachia ngazi. Nafasi ya Msemaji kwa sasa inabakia wazi na taratibu za kuijazi zitatangazwa hivi karibuni.

Stars yapata mechi

Taifa Stars itacheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Morocco mjini Marrakesh Septemba 5. Mchezo huo upo katika kalenda ya mechi za kimataifa za kirafiki za Shirikisho la Kandanda Duniani (Fifa) na tayari kocha mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij ametangaza kikosi cha wachezaji 26 watakaoingia kambini Agosti 31 tayari kwa mchezo huo.

Wachezaji hao ni Deogratius “Dida” Munishi (Young Africans), Mwadini Ali (Azam FC) ambao ni makipa wakati walinzi ni Oscar Joshua, Kelvin Yondani, Edward Charles na nahodha Nadir “Cannavaro” Haroub wote kutoka Yanga.

Walinzi wengine ni Saidi Moradi, Shomari Kapombe and Aggrey Morris (Azam), Joram Mgeveke (Simba) wakati viungo ni Erasto Nyoni, Himid Mao, Salum Abubakari (Azam), Saidi Ndemla (Simba), Mwinyi Kazimoto ((Markhiya, Qatar) na Saidi Juma wa Yanga.

Washambuliaji ni Simon Msuva, Mrisho Ngassa (Young Africans), John Bocco, Mcha Khamis (Azam), Juma Luizio (Zesco, Zambia), Mwegane Yeya (Mbeya City) na nyota wawili wa TP Mazembe, Mbwana Samattana Thomas Ulimwengu.

Mholanzi huyo alisema kuwa watawachuja wachezaji sita kabla ya kuondoka kwenda Morocco siku mbili kabla ya mchezo huo.