Sura mpya kikosi Yanga, inaweza kuwa na vikosi viwili vyenye uwepo wa Aziz Ki

Dar es Salaam. Wakati Yanga ikitangaza kumsajili mshambuliaji wa Asec Mimosas, Stephane Aziz Ki, vinara hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara pia wamekuwa pia na mikakati ya kumrudisha winga Bernard Morrison.

Yanga imeingia sokoni mapema kutokana na kutaka kumaliza usajili kwa ajili ya mashindano ya kimataifa, ambayo yataanza mapema na miamba hiyo kuanza hatua ya awali.

Kama usajili wa Yanga utakamilika kama walivyopanga, timu hiyo inaweza kuwa na sura na mwonekano huu.

Yanga inatarajiwa kuwa na kikosi cha kwanza kitakachokuwa na kipa Djigui Diarra, wakati Djuma Shaban na Kibwana Shomari wakiendelea karua ulinzi wa pembeni,

Katikati, Yanga inaweza kubaki na nahodha Bakari Mwamnyeto na Dickson Job, wakati kocha Nesreddine Nabi akitarajiwa kutumia viungo watatu kama alivyofanya kwenye mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FA (ASFC) dhidi ya Simba.

Katika mchezo huo, Nabi aliwatumia Khalid Aucho, Yannick Bangala na Feisal Salum ‘Feitoto’, wakati eneo la ushambulia, Fiston Mayele akisaidiwa na Aziz Ki na Morrison.

Kama timi itakuwa hicyo, mchambuzi wa masuala ya michezo nchini, Oscar Oscar alisema Ki ni moja kati ya vijaambao umri wake na uwezo ni faida kwenye timu, ingawa ameitaka Yanga isiweke matumaini ya kwamba atafika na kufunga mabao 20.

“Wampe muda, kwa kuwa bado anakuwa kisoka, asipewe mzigo mkubwa ingawa kiwango alichokionyesha kwenye timu aliyotoka ni cha kiwango cha juu, wanahitaji pia mshambuliaji wa kiwango cha Mayele,” alisema.

Jesse John, mchambuzi mwingine wa soka alisema msaada wa Ki Yanga itategemea na namna kocha atakavyomtumia, ingawa ana uzoefu wa kutosha katika soka.

“Nimeangalia video zake chache, yupo vizuri, hivyo itategemea na mfumo na namna kocha atakavyomchezesha,” alisema Jesse.