Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Straika Dodoma Jiji awekewa mkataba mpya mezani

DODOMA Pict

Muktasari:

  • Akizungumza na Mwanaspoti, mshambuliaji huyo alisema ni kweli yupo katika majadiliano ya kusaini mkataba mpya na kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao, ingawa hadi sasa hakuna makubaliano rasmi yaliyofikiwa kati yake na uongozi wa timu hiyo.

UONGOZI wa Dodoma Jiji uko katika mazungumzo ya kumuongezea mkataba mshambuliaji nyota wa kikosi hicho, Paul Peter, baada ya alionao sasa kufikia tamati mwishoni mwa msimu huu, lengo likiwa ni kumtaka aendelee kuichezea timu hiyo kwa miaka miwili.

Akizungumza na Mwanaspoti, mshambuliaji huyo alisema ni kweli yupo katika majadiliano ya kusaini mkataba mpya na kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao, ingawa hadi sasa hakuna makubaliano rasmi yaliyofikiwa kati yake na uongozi wa timu hiyo.

“Mkataba wangu unaisha msimu huu na tayari mazungumzo ya kuongeza mwingine yanaendelea, uliopo mezani ni wa miaka miwili zaidi wa kuendelea kuichezea Dodoma Jiji, ingawa suala la kubaki au kuondoka kwa sasa ni asilimia 50 kwa 50,” alisema.

Mbali na Dodoma Jiji kuhitaji kuendelea na nyota huyo, Mwanaspoti linatambua itakutana na ushindani kutoka kwa timu nyingine zinazohitaji saini yake, ingawa ameweka wazi kipaumbele cha kwanza ni sehemu anayoitumikia kwa sasa msimu huu.

Taarifa zinaeleza, Al Dahra Tripoli FC ya Libya bado inamuhitaji mshambuliaji huyo kwa ajili ya kuongeza nguvu, baada ya ofa ya kwanza waliyoiwasilisha Januari 2025, kugonga mwamba kwa kile kilichoelezwa waliwasilisha kiasi kidogo cha fedha.

Nyota huyo wa zamani aliyekulia akademi ya Azam FC kisha kupandishwa timu ya wakubwa, akiichezea pia KMC na Tanzania Prisons, amefunga mabao manane ya Ligi Kuu Bara na kuasisti mawili kati ya 30, yaliyofungwa na kikosi hicho msimu huu.