Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Stars kuivaa Benin bila mashabiki

Muktasari:

  • Timu zitakazoongoza makundi zitaingia hatua ya mwisho ya mtoano ambayo itatoa nchi tano zitakazofuzu Kombe la Dunia 2022

Mashabiki wa soka nchini hawatopata fursa ya kuingia uwanjani kutazama mechi baina ya Taifa Stars dhidi ya Benin kesho kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa 10 jioni

Mechi hiyo ni ya kundi J la kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika huko Qatar mwakani

Taarifa kutoka chanzo cha uhakika ndani ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) zimefichua kwamba Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limezuia mashabiki kuingia uwanjani katika mechi hiyo ya kesho

"Tuliomba mchezo huu turuhusiwe kuingiza mashabiki lakini ombi letu halijakubaliwa na CAF hivyo itachezwa bila mashabiki ambao watapata fursa ya kutazama kupitia luninga," kilisema chanzo hicho

CAF imekuwa ikizuia mashabiki kuingia viwanjani katika mechi za mashindano mbalimbali inayosimamia ingawa baadhi ya michezo imekuwa ikipewa ruhusa ya kuingiza idadi fulani kwa mashabiki

Stars inaongoza kundi J ikiwa na pointi nne sawa na Benin huku DR Congo yenye pointi mbili ikiwa na pointi mbili wakati Madagascar inashika mkia ikiwa haina pointi