Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Stand United yawaacha gizani wachezaji 8

Muktasari:

Timu hiyo ya mkoani Shinyanga ambayo inanolewa na Mrundi, Armas Niyongabo katika msimu uliopita ilimaliza ikiwa nafasi ya 11 kwa pointi 32, huku ikifanikiwa kufika nusu fainali ya Kombe la FA.

Shinyanga. Klabu ya Stand United ‘Chama la Wana’ imewafungulia mlango wa kutokea nyota wake nane, huku ikitangaza kikosi chake kipya kitakachotumika msimu ujao wa Ligi Kuu.

Timu hiyo ya mkoani Shinyanga ambayo inanolewa na Mrundi, Armas Niyongabo katika msimu uliopita ilimaliza ikiwa nafasi ya 11 kwa pointi 32, huku ikifanikiwa kufika nusu fainali ya Kombe la FA.

Akizungumza Mjini hapa, Mwenyekiti wa timu hiyo, Elyson Maheja aliwataja waliowaacha huru kuwa ni Hamad Kibopile, Salvatory Nkulila,  John Mwenda, Kisatya Sahani, Kitoba Emmanuel, John Lwitiko, Rajabu Rashid na Ally Mabrouk. 

Maheja alisema kuwa wachezaji wote hao wamemaliza mikataba yao na kwamba wengine kiwango chao kimepungua  na wanachohitaji ni ushindi msimu ujao.

Mwenyekiti huyo aliwataja pia waliosajiliwa kuwa ni.Makipa Mohamed Makaka, Philimon Mohamed, Mussa Mohamed, na Elias Sospiter,huku Mabeki ni Erick Mrilo, Juma Ally, Makenzi Kapinga, Niyonkuru Nassor na Bigirimana Ramadhan.

Wengine ni Ndoriyobija Erick,Jisendi Mathius,Ahmed Adewale,Ally Mohamed na Alfred Juma na Viungo ni Jacob Masawe, Mbiriz Erick, Bigirimana Brarse na Juventus Pastory.

Wamo pia Abdul Kasim,Yusuph Jamal,Paul Materaz,Salehe Lubili,Hafidh Mussa na Datius Piter,huku Washambuliaji wakiwa ni Sixtus Sabilo, Tariq shamte, Hakizimana Kitenge na Chinonsi Charles.

“Usajili wetu umezingatia sana mapendekezo ya Benchi la Ufundi katika kufikia malengo yetu,tunachotaka msimu ujao ni ushindi na tuna imani tutafanya vizuri”alisema Kiongozi huyo.