Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lwassa jeshi la mtu mmoja Kagera

LWASSA Pict

Muktasari:

  • Katika idadi hiyo ya mabao, vikosi hivyo vimeonekana kuwa na shida kubwa eneo hilo la ushambuliaji kiasi cha kuzinyima fursa ya kupata matokeo mazuri ambayo yangeziondoa na janga la kushuka.

KATIKA msimamo wa Ligi Kuu Bara, Kagera Sugar na KenGold zimeshuka daraja tayari huku timu hizo zikiwa ndiyo zenye idadi ndogo zaidi ya mabao ya kufunga ambayo ni 22 hadi sasa zikiwa zimecheza mechi 28 kila moja.

Katika idadi hiyo ya mabao, vikosi hivyo vimeonekana kuwa na shida kubwa eneo hilo la ushambuliaji kiasi cha kuzinyima fursa ya kupata matokeo mazuri ambayo yangeziondoa na janga la kushuka.

Hata hivyo, ukiangalia kikosi cha Kagera Sugar, inaonekana ilikuwa ni kama jeshi la mtu mmoja kufuatia Peter Lwasa kuwa na mabao manane peke yake, huku anayefuatia akifunga mawili ambao ni Cleophace Mkandala, Salehe Kambenga na Obrey Chirwa. Wenye moja ni Khasim Fekha, Tariq Seif, Datius Peter, Halifa Nolo, Mohamed Mussa Jecha, Saphan Siwa na Hija Shamte, wakati bao moja linalokamilisha idadi ya 22 likitokana na wapinzani kujifunga kupitia Ally Msangi wa Coastal Union.

Kwa upande wa KenGold iliyoshiriki Ligi Kuu Bara msimu huu kwa mara ya kwanza na kushuka, imebebwa kwa kiasi fulani na wachezaji watatu ambao kila mmoja amefunga mabao matano. Wachezaji hao ni Joshua Ibrahim, Selemani Bwenzi na Mishamo Michael. Hata hivyo, Herbert Lukindo amekuwa nyuma yao kwa ukaribu akifunga mabao manne, wakati Emmanuel Mpuka na Sadalah Lipangile kila mmoja akifunga bao moja. Lingine wapinzani walijifunga ambapo ni Yusuph Dunia wa Mashujaa.

Timu hizo katika kukamilisha msimu, zina mechi mbili kila moja zitakazochezwa Juni 18 na 22 mwaka huu ambapo Kagera Sugar zote itakuwa ugenini dhidi ya Namungo na Simba, huku KenGold ikiikaribisha Simba na kuifuata Namungo.