Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Staa Pogba aliposhindwa kumpa zawadi mwanaye

Muktasari:

  • Hata hivyo, mrembo huyo matata kutoka Bolivia hakutaka kumweka wazi mtoto wake, aliendelea kumfunikiza kumfisha asionekane na watu sura yake.

MANCHESTER, ENGLAND.DEMU wa kiungo, Paul Pogba yupo bize kwa sasa kumpeleka mtoto uwanjani Old Trafford kwenda kumwona baba akicheza kwa siku za karibuni.

Jumamosi iliyopita, mrembo Maria Salaues alimchukua mtoto wao aliyezaliwa hivi karibuni na kwenda uwanjani Old Trafford kumtazama Pogba alipokuwa akiitumikia Manchester United kwenye mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Southampton.

Katika mechi hiyo ambayo Man United ilishinda 3-2, Pogba ameshindwa kumpatia zawadi ya bao mwanaye baada ya kukosa mkwaju wake wa penalti katika dakika za mwisho za mchezo huo.

Mara ya kwanza, mrembo Maria Salaues alimpeleka mtoto huyo Jumapili ya wiki iliyopita wakati Man United ilipotoka sare ya bila kufungana dhidi ya Liverpool.

Hata hivyo, mrembo huyo matata kutoka Bolivia hakutaka kumweka wazi mtoto wake, aliendelea kumfunikiza kumfisha asionekane na watu sura yake.

Maria akiwa kwenye kivavi cha jeans ya denim na buti ndefu zilizofika hadi magotini, alihakikisha kwamba mwanaye anakuwa vizuri huku yeye mwenyewe akijikinga na hali ya hewa ya mwezi Machi huko England kwa kupiga jaketi la letha.

Mtoto huyo wa kwanza wa Pogba alizaliwa Januari na iliwekwa siri hadi hapo gwiji wa Man United, Bryan Robson kwa bahati mbaya alipofichua hilo kwa kumtumia salamu za pongezi kiungo huyo kwa kuwa baba. Baadaye, Pogba aliamua kuthibitisha kuwa baba wa mtoto wa kwanza.

Pogba na mrembo Maria wamekuwa wakiyafanya maisha yao kuwa siri kubwa kwani hata ile kufahamika tu Mfaransa huyo ana mchumba, basi ilifahamika kwenye fainali za Kombe la Dunia 2018 na timu ya staa huyo Ufaransa ilibeba ubingwa.

Pogba alikuja kuwafichulia watu kuna mtoto amezaliwa baada ya kufunga bao dhidi ya Brighton Januari na kisha kushangilia kwa kulipangusha tumbo lake.

Lakini, wiki iliyopita alishindwa kuweka nyavuni mbele ya mwanaye ambaye aliletwa uwanjani kumshuhudia baba yake akicheza.

Pogba amekuwa kwenye kiwango bora kabisa kwa sasa chini ya Kocha Ole Gunnar Solskjaer.