Srelio haitaki kurudia makosa

Muktasari:
- Ligi hiyo ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL), itaendelea kesho Jumamosi kwa michezo minane itakayochezwa kwenye Uwanja wa Donbosco Upanga unaotumika.
BAADA ya timu ya Srelio kupoteza michezo miwili ya kwanza, kocha wa timu hiyo Miyasi Nyamoko amesema kwa mechi dhidi ya maafande wa ABC hawatarudia makosa katika vita ya Ligi ya Kikapu ya Mkoa wa Dar es Salaam (BDL).
“Kwa kweli hadi tunafikia michezo tulizopoteza, tumeitana na tumejadiliana, ili kujua kitu kilichotungusha na tumeshajua sababu na sasa tunarudi kivingine,” alisema Nyamoko.
Hata hivyo, kufanya vibaya katika michezo hiyo, imeonyesha ni kutokana na kutokuwepo kwa wachezaji watatu wa kimataifa akiwamo Sponican Ngoma, Joseph Kamamba (Zambia) na Chaly Kasseng (Cameroun).
Srelio ilifungwa na Mchenga Star kwa pointi 82-70 kisha kulala kwa Dar City kwa pointi 105-32
Michezo mingine itakayochezwa leo upande wanawake ni kati ya DB Lioness na Mgulani JKT, Twalipo Queens na Real Dream na upande wanaume itakuwa kati ya Chui na Pazi.
Ligi hiyo ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL), itaendelea kesho Jumamosi kwa michezo minane itakayochezwa kwenye Uwanja wa Donbosco Upanga unaotumika.