Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Siri ya usajili wa Bui, Simchimba Geita Gold

Muktasari:

  • Benchi jipya la ufundi la Geita Gold inayojiandaa na Ligi ya Championship linaundwa na Amani Josiah, Choki Abeid (kocha msaidizi), Agustino Malindi (kocha wa makipa) na Paul Nonga (kocha wa viungo), usajili ilianza na Yusuph Mhilu aliyeongeza mkataba Julai 13, mwaka huu.

BAADA ya kukamilisha kuunda benchi la ufundi chini ya Kocha Mkuu, Amani Josiah, klabu ya Geita Gold imehamishia nguvu kusuka kikosi cha msimu ujao na imeanza kushusha majembe mapya iliyosajili kwenye dirisha kubwa la usajili.

Benchi jipya la ufundi la Geita Gold inayojiandaa na Ligi ya Championship linaundwa na Amani Josiah, Choki Abeid (kocha msaidizi), Agustino Malindi (kocha wa makipa) na Paul Nonga (kocha wa viungo), usajili ilianza na Yusuph Mhilu aliyeongeza mkataba Julai 13, mwaka huu.

Wiki hii klabu hiyo imekamilisha usajili wa nyota mbalimbali kutoka Ligi Kuu ambao imewatambulisha ni kiungo wa zamani wa Yanga na Kagera Sugar, Abdulaziz Makame na aliyekuwa mshambuliaji wa KMC na Ihefu, Andrew Simchimba.

Wengine ni beki wa zamani wa Yanga na Coastal Union, Adeyum Salehe, nyota wa zamani wa Mbeya City na Kagera Sugar, Gasper Mwaipasi, kiungo wa zamani Biashara United, Shaban Ada, Abdallah Madirisha na Mpapi Nasibu aliyewahi pia kukipiga Kagera Sugar.

Akizungumzia usajili huo, Mkurugenzi wa Mashindano Geita Gold, Liberatus Pastory, alisema kinachofanyika ni salamu kuonyesha namna walivyojipanga na kudhamiria kurudi Ligi Kuu ambayo walishuka msimu ulioisha.

"Usajili unaonyesha malengo ya timu ni ya aina gani na tumejipanga nia yetu ni kurudi Ligi Kuu, bado tunaendelea wengine bado wanakuja wachezaji hawa wengi ni wa Ligi Kuu siyo rahisi ina maana tumegharamika.

“Tayari tuko kambi tunaendelea na mazoezi kujiandaaa na ligi, tunafahamu kiu ya mashabiki wa Geita huu usajili na maandalizi mazuri ni kuirudisha timu ilipokuwa. Mashabiki wanaendelea kutuamini nasi tunaahidi kuwarudishia timu Ligi Kuu,” alisema Pastory