Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Singida BS yaichapa Mbeya City ikiisubiri Yanga vs Geita

Dodoma. Mchezo wa robo fainali ya mashindano ya Azam Sports Federation (ASFC)  kati ya Singida Big Stars dhidi ya Mbeya City umelizika katika uwanja wa Liti mkoani Singida kwa wenyeji kuibuka na ushindi wa mabao 4-1

Ilikuwa siku nzuri kazini kwa kiungo fundi Bruno Gomes ambaye katika mchezo huu amefunga  mabao mawili dakika za 7 na 57 huku mabao mengine yakifungwa na Bright  Adjei na Francy Kazadi katika dakika za 10 na 27.

Bao la kufutia machozi la  Mbeya City lilifungwa na mshabuliaji Eliud Ambokile dakika ya 55 ambaye aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Juma Shemvuni.  

SBS itasubiri mshindi kati ya  Yanga na Geita ambazo zinatarajiwa kucheza Aprili 8 mwaka huu katika uwanja wa Azam Complex Chamanzi Jijini Dar es salaam.

Mchezo wa nusu fainali kati ya SBS na mshindi kati ya Yanga na Geita Gold unatarajiwa kupigwa katika uwanja wa Liti mkoani Singida.


ZIFUATAZO NI DONDOO MUHIMU ZA MCHEZO HUU

Mbeya City haijawahi kupata ushindi katika michezo miwili iliyokutana kwenye ligi na SBS,mchezo wa mzunguko wa kwanza  uwanja wa Liti Mbeya City ilichapwa mabao 2-1 na mchezo wa pili zikatoka sare ya  bao 1-1 uwanja wa Sokoine Mbeya.

Katika mchezo huu,mwamuzi Ramadhan Kayoko kutokea Dar es salaam  alitoa kadi moja ya njano aliyomuonesha  Aziz Andambwile wa SBS  kutokana na kumchezea faulo Richardson Ng'odya.

Singida Big Stars tayari imejihakikishia kucheza kombe la Shirikisho barani Afrika  msimu ujao kwa kumaliza kwenye ‘top Four’ katika msimamo wa ligi Kuu Bara.

Katika mchezo huu winga wa SBS  Nickson Kibabage ametengeneza mabao mawili (Assist) kwa wachezaji Francy Kazadi na Bright Adjei kwenye dakika za 10 na 27.

Winga wa Mbeya City,Richardson Ng’odya anashika nafasi ya tatu kwa ufungaji akiwa na mabao matano huku  Andrew Simchimbi wa Ihefu akiongoza akiwa na mabao saba akifuatiwa na Clement Mzize wa Yanga  mwenye mabao sita.

Kocha wa SBS aliwatoa Bruno Gomes,Nickson  Kibabage,Bright Adjei,  Paschal Wawa na Francy Kazadi  na nafasi zao  zilichukuliwa na Deus Kaseke,Nasoro Saadun, Amiss Tambwe,Hamad Waziri na Rodrigue Tegu.

Kwa upande wake Kocha wa Mbeya City,Mubiru Abdallah aliwaingiza Hassan Machezo,Eliud Ambokile na George Sangija na kuwatoa  Awadh Juma, Baraka Mwalubunju na Juma Shemvuni.

Mbeya City hiyo ndio mara yake ya kwanza kutinga hatua ya robo fainali tangu ilipopanda daraja msimu wa 2013-2014 mara zote imekuwa ikiondolewa hatua za awali.

Mapema dakika ya 6 beki wa Mbeya City,Samson Madeleka aliumia  na kukimbizwa Hospitali wakati akimdhibiti Kibabage asilete madhara na nafasi yake ilichukuliwa na Hassan Mohammed.