Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Singida Black Stars katikati ya mtego

SINGIDA Pict

Muktasari:

  • Ushindi wa Singida ni wa kisasi baada ya kikosi hicho kupoteza mechi mbili za Ligi Kuu Bara, ikianza na kuchapwa bao 1-0, Desemba 28, 2024, huku raundi ya pili iliyopigwa Mei 28, 2025, kwenye Uwanja wa KMC Complex Mwenge ikachapwa tena 1-0.

MICHUANO ya Kombe la Shirikisho (FA), imefikia patamu ambapo tumeshuhudia timu mbili zikikata tiketi ya kucheza fainali, ikianza Yanga iliyoichapa JKT Tanzania mabao 2-0, kisha Singida Black Stars ikafuzu pia kibabe kwa kuicharaza Simba 3-1.

Ushindi wa Singida ni wa kisasi baada ya kikosi hicho kupoteza mechi mbili za Ligi Kuu Bara, ikianza na kuchapwa bao 1-0, Desemba 28, 2024, huku raundi ya pili iliyopigwa Mei 28, 2025, kwenye Uwanja wa KMC Complex Mwenge ikachapwa tena 1-0.

Licha ya kisasi hicho, ila Singida inakabiliwa na rekodi ngumu ya kuivunja, kwani michuano hiyo iliporejea tena msimu wa 2015-2016, baada ya kutofanyika kwa kipindi cha miaka 13, tangu mwaka 2002, hakuna timu iliyochukua ubingwa huo zaidi ya Yanga.

Timu nyingine zilizochukua ubingwa huo tangu kipindi hicho mbali na Yanga ni Simba, Mtibwa Sugar na Azam FC ambazo zote tayari zimetolewa, jambo linalosubiriwa pia kuona kama Singida Black Stars itaandika rekodi mpya au itashindwa kutamba.

Tangu michuano hiyo iliporejea tena msimu wa 2015-2016, Yanga ndio timu inayoongoza kwa kuchukua ubingwa huo mara nyingi zaidi, baada ya kufanya hivyo mara nne, ikifuatiwa na wapinzani wao wakubwa Simba, waliolichukua taji hilo mara tatu.

Singida ilianza michuano hiyo hatua ya 64, bora kwa kuifunga Magnet FC zamani Malimao ya Dar es Salaam mabao 2-0, kisha 32, bora ikakutana na Mabingwa wa Mkoa wa Kagera, Leo Tena FC na kuichapa mabao 4-0 na kufuzu kibabe katika hatua ya 16, bora.

Hatua ya 16 bora, Singida ikakutana na KMC FC inayoshiriki Ligi Kuu Bara na kuichapa bao 1-0, huku hatua ya robo fainali ikaichapa Kagera Sugar mabao 2-0 na kufuzu nusu fainali, kisha kuiondosha Simba kwa kuifunga 3-1 na kutinga fainali.

Jambo moja la kipekee kwa Singida, tangu michuano hiyo imeanza msimu huu, imeruhusu bao moja tu ambalo ni la kiungo wa Simba, Jean Charles Ahoua, huku kwa upande wa wapinzani wao Yanga ikiwa hadi sasa imeruhusu nyavu zake kutikiswa mara mbili.

Mbali na hilo, Singida inakabiliwa na mtihani wa kuvunja rekodi ya Yanga ya kutopoteza mechi ya Kombe la Shirikisho la (FA), kwani kikosi hicho tangu mara ya mwisho kilipochapwa na Simba bao 1-0, Julai 25, 2021, hadi leo hakijapoteza.

Fainali hiyo iliyoshuhudiwa Simba ikitwaa ubingwa huo kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika Kigoma kwa bao la kiungo wa zamani wa kikosi hicho, Mganda Taddeo Lwanga, ni kama iliipa hasira Yanga kwani hadi leo imecheza mechi 23, bila ya kupoteza.

Kichapo hicho pia, kikaifanya Yanga kutwaa ubingwa wa michuano hiyo mara tatu mfululizo kuanzia msimu wa 2021-2022, hadi sasa, jambo linalosubiriwa pia kuona kama Singida itaivunja rekodi katika fainali itakayopigwa kati ya Juni 26 hadi 28.