Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simbu aingia kumi bora RAK Half Marathon

Mwanariadha nyota wa Tanzania, Alfonce Felex Simbu amefanikiwa kuingia katika nafasi kumi bora katika michuano ya kimataifa ya RAK Half Marathon yaliyofanyika nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Mashindano hayo yaliyomalizika hivi punde, Simbu amefanikiwa kuipeperusha vema bendera ya Tanzania mbele ya maelfu ya magwiji wa mchezo wa riadha walioshiriki mashindano hayo kutoka katika kila pembe ya dunia.

Mashindano ya RAK Half Marathon yamekatwa utepe wa ushindi na mwanariadha Jacob Kiplimo kutoka Ugandaa aliyetumia dakika 57:56, kumaliza mbio.

Nafasi ya pili katika mashindano hayo imechukuliwa na  Rodgers Kwemoi  aliyemaliza kwa Dakika 58:30, huku nafasi ya tatu akichukua Kenneth Kiprop Renju aliyetumia dakika 58:35, wote kutoka Kenya.

Nafasi ya nne hadi 10 zimechukuliwa na  Seifu Tura Abdiwak (58:36),  Amdework Walelegn Tadese(58:40,  wote kutoka Ethiopia, Daniel Kibet Mateiko (58:45), Alexander Mutiso Munyao (58:48)  nafasi nane akishika Abel Kipchumba( 59:47), wote kutoka Kenya wakifuatiwa na  Alphonce Felix Simbu  (1:00:03) na naafsi ya kumi ni Kennedy Kimutai (1:00:10) kutoka Kenya.

Katika mashindano hayo Tanzania iliwakilishwa na wanariadha watatu mwingine akiwemo Faraja Damas aliyemaliza katika nafasi ya 20 akitumia saa 1:03:4.

Mwanadada pekee aliyeipeperusha bendera ya Tanzania katika mashindano hayo ni Jackline Sakilu aliyetumia saa1:15:38